Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (katikati), wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi
Leonard Masanja, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji nchini( EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje, wa Pili kulia,
wakionyeshwa Tanki la kuhifadhia mafuta katika moja ya vituo vya mafuta
alivyovikagua wakati wa ziara yake iliyofanyika Aprili 20, 2021.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani amepiga marufu uuzaji wa mafuta ya Petroli, Dieseli, na Mafuta ya Taa yasiyo
na vinasaba unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara nchini.
Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo Jijini
Dodoma wakati wa ziara yake ya kushtukiza ya kukagua vinasaba kwenye mafuta
yaliyopo katika vituo vya kuuzia mafuta mkoani humo, iliyofanyika Aprili 20,
2021.
Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, Naibu Katibu Mkuu, Kheri
Mahimbali na Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi wa wizara hiyo, pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka wa Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini(
EWURA),Mhandisi Godfrey Chibulunje.
Dkt. Kalemani Alisema kuwa vinasaba
vinadhihirisha viwango na ubora wa mafuta nchini.
“Maelekezo yangu kwa wauzaji wa mafua
nchini ni lazima muendelee kuuza mafuta yenye vinasaba kwa sasa ili
kujiridhisha na kiwango na ubora wa mafuta nchini, na kama mafuta hayana
vinasaba ni marufuku kuyachukuwa na kuuza, kuna minong’ono katika baadhi ya
maeneo kuwa kuna mafuta yanayouzwa ya aina hiyo, tutakayembaini tutachukua
hatua stahiki”, alisema Dkt. Kalemani.
Katika ziara hiyo, hakuna kituo hata
kimoja kilichobaininika kuuza mafuta yasiyo na vinasaba.
Alieleza kuwa kwa sasa Shirika la
Viwango nchini (TBS), ndiyo llililopewa kazi ya kupima na kuweka vinasaba
katika mafuta yote yanayoingia nchini ili kudhibiti ubora na tayari kazi hiyo
imeanza kufanyika.
Alisisitiza kuwa kuanzia sasa mafuta
yote nchini yatakuwa yakipimwa na kuwekwa vinasaba na TBS na ikibainika kuna
mafuta ambayo hana vinasaba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watendaji
husika.
“TBS ni chombo cha serikali, kinachofanya
kazi ya kudhibiti ubora na viwango ikiwepo wa mafuta nchini hivyo kuanzia sasa
ndiyo kifanya kazi ya kupima na kuweka vinasaba kwenye mafuta yote nchini, endapo
atatokea mwingine mtaelekezwa na serikali”, alisisitiza Dkt. Kalemani.
Lengo la serikali kuipa TBS kazi ya
kuweka vinasaba katika mafuta yote nchini ili kuokoa fedha za serikali zaidi ya
shilingi bilioni tatu kwa mwezi ambazo awali alikuwa akilipwa aliyekuwa
akifanya kazi hiyo.
Vilevile ni kuijengea uwezo taasisi
hiyo na kuongeza ajira kwa watanzania.
Katika ziara hiyo, aliitoa maelekezo
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Wizara ya Maji kuwachukulia hatua waafisa
wawili katika idara ya manunuzi wa Mamlaka wa Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji nchini( EWURA), pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi wa taasisi hiyo kwa
kushindwa kutekeleza maelekezo ya serikali kwa wakati.
Dkt. Kalemani alisema kuwa watumishi hao, hawakutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa tangu Februari 5, 2021, kwa sababu zao wenyewe, pia wachunguzwe kwa nini hawakutekeleza maagizo hayo, na kusababisha migogoro.
0 comments:
Post a Comment