WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini
kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.
Pia Waziri Mkuu amesema Serikali
imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto
wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana
(Jumatano, Oktoba 04, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya
Sekondari ya Wasichana na WAMA Sharaf.
Shule ambayo ipo wilayani Lindi
inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo inasomesha watoto wa kike ambao ni
yatima na wanaotoka katika mazingira magumu.
Waziri Mkuu amewataka wanafunzi
hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii
na hatimaye watimize malengo yao.
Amesema ni vema wanafunzi hao
wakatumia vizuri fursa hiyo ya elimu wanayoipata shuleni hapo kwa kusoma
kwa bidii na wafuate ratiba itakayokuwa inapangwa.
“Nawasihi mtumie muda huu kusoma
kwa bidii ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae.
Msikubali kushawishika na kukatisha masomo yenu.”
Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya
WAMA, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Kuteuliwa alisema shule
hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu
kutoka mikoa yote nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 05, 2017.
0 comments:
Post a Comment