Mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,wakati wa makabidhiano ya pikipiki kumi kwa maafisa mifugo katika halmashauri ya Chalinze kwa lengo la kufikia wafugaji kuwapa elimu za kufuga kisasa na kuondokana na migogoro na wakulima,makabidhiano yaliyofanyika huko Lugoba.(picha zote na Mwamvua Mwinyi )
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE wa jimbo la Chalinze
,Ridhiwani Kikwete,amekabidhi pikipiki kumi ,zilizogharimu sh.Mil.22.5
kwa maafisa mifugo wa kata ,ili waweze kuwafikia wafugaji wote,kupeleka
sera ya kufuga kisasa na kuondoa migogoro na wakulima.
Aidha amekemea tabia inayofanywa
na baadhi ya wafugaji ya kufuga kizamani kwa kuswaga makundi ya ng’ombe
kwenye eneo moja hali inayosababisha kuharibu rutuba.
Akikabidhi pikipiki hizo,huko
Lugoba Ridhiwani alieleza , vyombo hivyo vya usafiri vikatumike
kusimamia majukumu waliyonayo badala ya kuvitumia kwa matumizi yao
binafsi.
Aliwataka jamii ya wafugaji
kuachana na mtazamo hasi wa kufuga kizamani mifugo lundo isiyo na tija
pamoja na kuingia katika maeneo ambayo hayajatengwa kwa ajili yao.
“Sisi hapa ni kazi tuu mkasimamie
majukumu yenu ipasavyo ili kuondokana na changamoto zinazowakabili
wafugaji na muwafikie wanannchi muwaeleze juu ya ufugaji bora “
“Eneo zima linageuzwa
machungio,wafugaji wafuge kwa kuheshimiana hivyo muwafikie walio mbali
muwape elimu hasa ya ufugaji bora.visingizio vimekwisha kuwa hamna
usafiri, matarajio yangu ni mtaenda kutekeleza ilani ya CCM”alisema
Ridhiwani.
Ridhiwani ,alieleza wafugaji hasa
wa kimasai wanaamini kuwa na ng’ombe wengi ndio utajiri ,waondoe dhana
hiyo kwani sio sifa,wajaribu kufuga mifugo michache na kujiwekea kasumba
ya kufuga kwenye mazizi.
Hata hivyo ,alimpongeza mkurugenzi
wa halmashauri ya Chalinze,Edes Lukoa kwa kusimamia na kuyafanyia kazi
maazimio ya madiwani ambayo huwa wakitoa .
Ridhiwani,alito mafuta lita tano
kwa kila pikipiki na kuahidi kuangalia uwezekano wa kufanya utaratibu
kila mwezi kwenye posho zinazokwenda katika kata maafisa mifugo hao
wataongeza japo 5,000 kwa ajili ya mafuta ya pikipiki hizo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
halmashauri hiyo,Lukoa alisema pikipiki hizo zimenunuliwa kutokana na
mapato ya ndani ya halmashauri .
Alizitaja kata zilizokabidhiwa
usafiri huo kuwa ni sanjali na
Vigwaza,Kibindu,Mbwewe,Talawanda,Msata,Kimange,Kiwangwa,Miono,Ubena
Zomozi na Mandela.
Lukoa alieleza kwa msimu wa
bajeti 2017/2018 wanatarajia kununua pikipiki nyingine 15 kwa ajili ya
watendaji na nyingine nane kwa ajili ya maafisa mifugo wa kata na vijiji
.
Aliwashukuru madiwani kwa
ushirikiano na CMT kwa mchango wao mkubwa katika kutoa maazimio
yaliyotakiwa yatekelezwe na halmashauri na sasa yamefanikiwa.
Lukoa alifafanua,kila afisa mifugo
wa kata anayekabidhiwa pikipiki atasaini mkataba wa makubaliano na
mwajiri wake na atatakiwa kuchangia asilimia 50 ambayo ni sawa na sh.bil
1.125 ya sh.bil 2.250 ambayo ni bei ya kukunuliwa atakayokabidhiwa kwa
kipindi cha miaka mitano.
“Hali hiyo itasaidia kutunza
pikipiki kwa kuwa itakuwa ni mali yao baada ya kumaliza kuilipia malipo
wanayokatwa yatawezesha kununua pikipiki nyingine ili kuimarisha huduma
za ugani’alisema Lukoa.
Nae afisa mifugo na kilimo katika
halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo Issack Kama,alisema wapo maafisa
mifugo wa kata na vijiji 26 ambao wanapaswa kutoa huduma za ushauri wa
kitaalamu kwa wafugaji waliopo kwenye vijiji 68 vilivyopo humo .
Alibainisha kati ya maafisa hao
wanne pekee ndiyo wana pikipiki na wengine 22 hawana hali iliyokuwa
ikisababisha kushindwa kuwafikia wafugaji na kuwapa huduma
zinazostahili.
Kama alisema ili wafugaji waweze
kupata mafanikio katika ufugaji wanapaswa kufuata kanuni bora za ufugaji
kupitia ushauri wa maafisa mifugo wa kata na vijiji.
Katika hatua nyingine,baadhi ya
maafisa mifugo waliokabidhiwa vyombo hivyo vya usafiri akiwemo afisa
mifugo kata ya Talawanda Enerst Lesi,wa kata ya Mbwewe Rashid Mdemu
walishukuru kupata pikipiki hizo kuwafikia wafugaji na kuboresha huduma
za ugani ukizingatia wafugaji wengi wanakaa mbali.
Mdemu alielezea,kata ya Mbwewe ina
vijiji sita hivyo ilikuwa ni vigumu kuvifikia vyote hasa katika kutoa
elimu mbalimbali na kufanikisha zoezi la kupiga alama (chapa)mifugo ili
iwe rahisi kutambulika.
Akitoa shukrani ya pamoja afisa mifugo kata ya Msata,Agripina Silau ,alisema usafiri huo wameupokea katika muda muafaka .
Alimhakikishia mbunge huyo kuwa
watakwenda kuwajibika kikamilifu ili kuleta mabadiliko na kutatua
changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji licha ya kwasasa
kuonekana kuanza kupungua.
Usajili wa mifugo na kuweka alama kwenye mifugo usafiri huu umekuja muda muafaka.
Kwa mujibu wa sense ya mifugo ya
mwaka 2012,halmashauri ya Chalinze ina jumla ya ng’ombe 240,000,mbuzi
94,000,kondoo 54,000,kuku 380,000 na wanyama wengine.
0 comments:
Post a Comment