Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imetembelea mpaka wa nchi ya Tanzania na Uganda
Akizungumza mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Nape Nnauye amesema kuwa lengo la ziara ya Kamati yake lilikuwa ni kujiridhisha na mahitaji ya kuboresha na kuimarisha mipaka kutokana na alama za mipaka (BEACON) zilizopo sasa kuwa chache na kukaa mbalimbali
'... Tumefanya ukaguzi katika mipaka ya nchi yetu na wenzetu wa Uganda, Miongoni mwa tulichobaini ni uhitaji mkubwa wa maboresho ya mipaka yetu kwani zile alama za mipaka ya nchi (beacon) ziko mbalimbali na chache ...' Alisema
Mwenyekiti huyo pia aliwataka wananchi wa eneo hilo kusogea ili kuacha nafasi ya kuwepo kwa eneo wazi
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyeambatana na Kamati hiyo Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa zoezi la uboreshaji wa mpaka huo linatarijiwa kuanza hivi karibuni na kuongeza kuwa Serikali itahakikisha inatoa elimu kwa wananchi juu ya ulinzi wa mipaka na umuhimu wa kuacha eneo la wazi ili kuepusha mwingiliano wa pande zote mbili sambamba na kuongeza kuwa Serikali ilishatenga kiasi cha fedha shilingi bilioni 4 kati yake bilioni 1.9 zitatumika katika kuboresha mpaka wa Uganda na Tanzania, Na shilingi bilioni 2.1 kuboresha mpaka wa Tanzania na Kenya na teyari Serikali imeshatoa pesa zote kwaajili ya kazi hiyo
Akihitimisha mkurugenzi wa upimaji na ramani wa wizara ya ardhi nchini amefafanua kuwa vipo vikwazo vingi katika uhimilishaji wa mipaka moja wapo ikiwa ni nchi kutokuwa tayari pale inapoanzisha zoezi hilo
Kamati hiyo pia ilimpongeza na kumshukuru mkuu wa wilaya ya Misenyi, Mhe Kanali Dennis Mwira kwa kazi nzuri anayoifanya ya kulinda mipaka ya nchi na kuendelea kudumisha usalama wa raia na mali zao
'... Hapa Kazi Tu ...'
0 comments:
Post a Comment