Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya Kilimo Dkt.Wilhelm Mafuru akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu
Wajumbe wa kikao cha Kutathmnini Mpango wa Kilimo wa Kuhimili Mabadiliko ya tabia nchi mara baada ya ufunguzi Jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa kikao cha Kutathmnini Mpango wa Kilimo wa Kuhimili Mabadiliko ya tabia nchi mara baada ya ufunguzi Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew
Mtigumwe amewapongeza wadau wa maendeleo wa ndani na nje kwa kufanikisha Mpango
wa Kilimo wa Kuhimili Mabadiliko ya tabia nchi (ACRP)
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Dkt.Wilhelm Mafuru Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti Wizara ya
Kilimo alipofungua kikao cha tathmni ya Mpango kwa niaba ya Katibu Mkuu
"Wizara ya Kilimo imefanikisha
Mpango huu wa Kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhamasisha Kilimo
kinachojali na kulinda mazingira kwa ushirikiano na wadau" alisema Dkt
Mafuru
Aliongeza kusema Mpango huo ulianza
kutekelezwa na Wizara mwaka 2014 na unafikia mwisho mwaka huu 2019 ambapo lengo
kuu la Mpango lilikuwa kuhakikisha nchi inaongeza uzalishaji wa mazao na
usalama wa chakula.
Mpango huu unahamasisha wakulima
kutumia eneo dogo kuzalisha mazao mengi kwa tija wakizingatia matumizi sahihi
ya teknolojia na hifadhi ya mazingira .
Dkt.Mafuru ametaja maeneo ya kipaumbele
yaliyotekelezwa kwenye Mpango wa kilimo cha Kuhimili mabadiliko ya tabia nchi
(ACRP) kuwa ni kuboresha matumizi ya ardhi na maji,kuchochea matumizi ya Kilimo
kinachokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na tatu kupunguza madhara ya
athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Utekelezaji huu wa Mpango umezingatia
Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025),Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ( 2020) na
Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).
Naye Mshauri wa Mazingira na Uhifadhi
wa Mali asili toka Ubalozi wa Norway nchini Ingvild Langhus amesema Kilimo
kinachohilimi mabadiliko ya tabia nchi kinasaidia kuondoa uchafuzi wa hali ya
hewa na mazingira.
Amesema Norway kwa zaidi ya miaka
Arobaini imekuwa ikishirikiana na serikali ya Tanzania katika kuinua sekta ya
Kilimo hususan utafiti.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa kitengo
cha Mazingira Wizara ya Kilimo Prosper Makundi amesema Mpango huu kutokana na
mafanikio yaliyofikiwa nchini ni budi wadau na wahisani wakaona namna ya
kuongeza ufadhili ili awamu ya pili ya ACRP ianze.
"Baada ya kikao hiki ni
mategemeo ya wizara kuona wadau wetu wanaongeza ufadhili ili kazi ya kusimamia
na kuelimisha wakulima kilimo kinachohilimi mazingira iendelee awamu ya
pili" alisema Makundi.
Kikao kimeandaliwa na.Wizara ya Kilimo
na kushirikisha na wadau toka Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mazingira.Wizara ya
Ardhi.SUA,FAO,WB,Care International, FORUMCC,IITA na ANSAF
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment