Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akikagua ofisi mpya za Bodi ya Mkonge jijini mara baada ya kutekelezwa kwa agizo la Waziri Mkuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyevaa tai) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao Bw.Nyasebwa Enock kuhusu bodi ya mazao kuweka bango la ofisi eneo hilo.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw.Saad Kambona
Picha ya pamoja kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( aliyevaa tai) na Menejimenti ya Bodi ya Mkonge mara baada ya kukagua jengo la ofisi kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kuitaka bodi ihamie hapo toka ofisi za zamani uwanja wa gofu jijini Tanga. Jengo hilo awali lilifahamika kama Medicare Hospital Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martin Shigela (katikati) akiongoza mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo kuhusu mkakati wa kuinua zao la mkonge mkoa wa Tanga.Mazungumzo yalifanyika jana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyevaa suti ya kaki) akiangalia bango litakalowekwa katika jengo jipya la makao makuu ya bodi ya mkonge jijini Tanga ambalo zamani lillifahamika kama Medicare Hospital Tanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiongea na watumishi wa Bodi ya Mkonge wakati alipotembelea makao makuu ya bodi hiyo jijini Tanga jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya
ameipongeza Menejimenti ya Bodi ya Mkonge na watumishi kwa kutekeleza agizo la
Waziri Mkuu la kuhamia katika ofisi iliyotwaliwa na serikali hivi karibuni
kutoka kwa wamiliki binafsi.
Kusaya ametoa pongezi hizo jana (tarehe
27.O4.2020) Jijini Tanga wakati alipokwenda kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji
wa maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu mwezi Machi mwaka huu kufuatia ripoti ya
kamati ya uchunguzi kuhusu mali za bodi ya mkonge kumilikishwa kwa watu binasfi
kinyume cha utaratibu.
“Nawapongeza menejimenti mpya ya Bodi ya Mkonge
kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuhamia
katika jengo hili na kuendelea na kazi za kusimamia zao la mkonge”alisema
Kusaya
Waziri Mkuu aliagiza kuwa jengo lililokuwa
linamilikiwa visivyo halali na Willian Kimweli Madundo na kulitumia kama
Medicare hospital Tanga litumike kuwa makao makuu ya bodi kwani miaka ya nyuma
ndipo palikuwa makao makuu ya Mamlaka ya Mkonge Tanzania .
Aidha,Katibu Mkuu huyo aliigiza bodi ya mkonge
kuhakikisha inafuatilia mali zake ikiwemo nyumba 32 ambazo zilirejeshwa
serikalini “ nataka waliokuwa wamiliki wapewe notisi na kuondoka au wapewe
mikataba ya upangaji haraka” alisisitiza
“Bado kuna nyumba mbili nchini Uingereza,nataka
zirejeshwe serikalini na zile nyumba mbili jirani na Mkonge hotel hapa Tanga
zifuatiliwe kujua uhalali wa umiliki wake “ alisema Katibu Mkuu huyo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi
ya Mkonge Saad Kambona alimweleza Katibu Mkuu kuwa tayari wameanza kufanya kazi
kwenye jengo jipya la ofisi kama walivyoagizwa na wamefanya ukarabati mdogo
kuwezesha jengo hilo kutumika kama ofisi badala ya ofisi za zamani uwanja wa
gofu Tanga .
Kambona alisema kwa sasa wanaiomba serikali
kuendelea kuiwezesha bodi ili iweze kuhudumia zao la mkonge wakati ikijipanga
kuanza kujitegemea kimapato.
‘Tuna lengo baada ya kuimarisha usimamizi wa
zao la mkonge nchini,bodi iweze kutoa gawio kwa serikali “alisema Kambona.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martin Shigela aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa jitihada zake za kufufua zao la
mkonge kwani ndio uti wa mgongo wawananchi wa Tanga.
Shigela alisema ni wakati sasa wizara ya kilimo
ikaongeza msukumo katika kuhakikisha mbegu za mkonge zinapatikana kwa wingi na
wakulima wanazipata kwa gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment