Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani( kulia) akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Busomeke( katikati)
wilayani Igunga mkoani Tabora baada ya waziri huyo kuwasha umeme katika nyumba
mwanakijiji huyo.
Moja ya nyumba iliyowashiwa umeme
katika Kijiji cha Busomeke wilayani Igunga mkoani Tabora baada ya Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani kufanya ziara ya kukagua shughuli za usambazaji
umeme Vijijini wilayani humo Aprili 27, 2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani akizungumza na Viongozi wa Kijiji cha Busomeke katika Wilaya ya Igunga
mkoani Tabora, alipofanya ziara ya kukagua shughuli za usambazaji umeme
vjijini, Aprili 27, 2020.
Viongozi wa Kijiji cha Mizanza
wilayani Igunga Mkoani Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,
hayupo pichani baada ya kufanya ziara kijijini hapo ya kukagua shughuli za
usambazaji umeme vjijini, Aprili 27, 2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani( katikati)akizungumza na Viongozi wa Kijiji cha Mizanza katika Wilaya
ya Igunga mkoani Tabora, alipofanya ziara ya kukagua shughuli za usambazaji
umeme vjijini, Aprili 27, 2020.
Mbunge wa Manonga, Saif Gulamali
(katikati) akizungumza na Viongozi wa Kijiji cha Mizanza katika Wilaya ya
Igunga mkoani Tabora, alipofanya ziara ya kukagua shughuli za usambazaji umeme
vjijini, Aprili 27, 2020. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kuongeza kasi ya kutumia umeme
unaopatikana mkoani humo kwakuwa matumizi yao yapo chini zaidi kulinganisha na
umeme unaozalishwa mkoani humo.
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati
akikagua shughuli za usambazaji wa umeme vijijini katika Kijiji cha Mizanza na
kuwasha umeme katika Kijiji cha Busomeke wilayani Igunga mkoani Tabora, Aprili
27, 2020.
Dkt. Kalemani alisema kuwa
mitambo ya kufua umeme iliyopo mkoani humo inauwezo wakuzalisha Megawati 42 za
umeme ili itumike mkoa mzima lakini mpaka sasa matumizi ni Megawati 14 tu.
“Kwa nini ninyi wakazi wa Tabora
hamtaki kutumia umeme haliyakuwa tayari miundombinu imewafikia na bei ya
kuunganisha ni 27,000 tu! mitambo ya hapa Tabora inauwezo wa kufua umeme wa
Megawati 42, ninyi matumizi yenu hayafiki hata nusu ya umeme huo,hii si sawa
mtaharibu mitambo yetu kwakuwa mingine italazimika kuzimwa na ikizimwa kwa muda
mrefu itaharibika na nchi itapata hasara” alisema Dkt. Kalemani.
Aliwataka Viongozi wa Serikali za
Vijiji, Mitaa pamoja na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuongeza kasi ya
kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kuunganisha umeme katika nyumba zao.
Vilevile aliwataka wananchi hao
kuongeza shughuli za uzalishaji mali kama vile viwanda vidogo vinavyotumia
umeme ili kuongeza idadi ya matumizi ya umeme ambao mwingi hupotea kwa kukosa
watumiaji hali yakuwa bado wakazi wengi hawana huduma hiyo.
Katika ziara yake hiyo, aliwasha
umeme katika Kijiji cha Busomeke na kuwataka wananchi wa eneo hilo kuendelea
kulipia shilingi 27,000 ili waunganishiwe umeme.
Akiwa katika Kijiji cha Mizanza,
Dkt. Kalemani aliiagiza TANESCO, kuharakisha upelekaji wa nguzo kijijini hapo,
ili kuwapa fursa wakazi wa kijiji hicho kuunganishiwa umeme, hivyo amewataka
wakazi hao kulipia gharama za
uunganishwaji na kutandaza nyaya katika nyumba zao.
Aliendelea kusisitiza kuwa miradi
ya usambazi umeme vijiji hauna fidia, hivyo wananchi watoe ushirikiano kwa
wakandarasi na TANESCO pindi wanapopitisha miundombinu katika maeneo yao kwa
lengo la kurahisisha utekelezaji wa kazi hiyo.
Hata hivyo aliwataka kutumia
wakandarasi walioainishwa na TANESCO na wanaotambulika katika serikali za mitaa
na vijiji vyao ili kuepuka vishoka na watu wasiowaaminifu.
Sambasamba na hilo, aliwaeleza
kuwa wasikubali kulipia miundombinu ya umeme kama nguzo, nyaya, mashineumba
(Transfoma) wala mita za LUKU.
0 comments:
Post a Comment