Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amekasirishwa na utekelezaji wa miradi ya Afya katika Mkoa nzima wa Mtwara.
Hilo limetokea wakati wa ziara ya Waziri huyo Mkoani humo alipo tembelea katika halmashauri mbalimbali za Mkoa huo.
Akihitimisha ziara yake katika kituo cha Afya Kilambo katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara Jafo alikuta ujenzi wa kituo hicho ambacho kilipokea fedha tangu mwaka jana 2018 kikiwa bado hakija kamilika. Ikumbukwe kwamba ziara hiyo ilianzia katika halmashauri za Nanyumba na Masasi ambapo zote zilibainika kuwa na shida katika utekelezaji wa miradi ya Afya.
Jafo alisema kwamba Mkoa huo umeonekana umekuwa na usimamizi usio ridhisha wa miradi ya Afya iliyo elekezwa katika Mkoa huo. Jafo ametoa maelekezo kwamba kituo cha Afya Kilambo kiwe kimekamilila ifikapo January 15, 2020.
Aidha, Jafo alitembelea mradi wa Soko la Kisasa linalo jengwa ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
0 comments:
Post a Comment