Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na mjasiriamali Bi Winifrida Nzunda wakati alipotembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali wauzaji wa mchele katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe juzi tarehe 21 Novemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wanawake wajasiriamali wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati alipotembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali wauzaji wa mchele katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe juzi tarehe 21 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na wana kikundi cha wanawake wajasiriamali wauzaji wa mchele katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe juzi tarehe 21 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na wana kikundi cha wanawake wajasiriamali wauzaji wa mchele katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe juzi tarehe 21 Novemba 2019.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Songwe
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa
serikali haiwezi kupanga bei elekezi ya mchele ama mahindi hivyo amewataka
wakulima kote nchini kupandisha bei ya mazao hayo kadri wawezavyo kulingana na
mahitaji ya soko.
Akizungumza wakati alipotembelea kikundi cha wanawake
wajasiriamali wauzaji wa mchele katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe juzi tarehe
21 Novemba 2019 alisema kuwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya nafaka
ambayo ni mahindi na mchele katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 waendelee
kunufaika na biashara ya mazao hayo kulingana na mahitaji ya soko.
Alisema kuwa wakati bei ya mazao hayo inaposhuka
sokoni serikali haiingilii kupandisha bei ya mazao hayo na wananchi hufurahia
kushuka kwa bei, hivyo basi wakati bei ikipanda pia wakulima wanatakiwa
kuendelea kufurahia na kununua kwa wingi mazao hayo.
“Kuna watu wananipigia simu wakidai mishahara iongezwe
kwa watumishi kwakuwa bei za mahindi na mchele zimepanda, na mimi nimekuwa nikiwajibu
wakati bei ikipungua mbona hawajawahi kunipigia wakiniomba mishahara ipunguzwe”
Alihoji Mhe Hasunga
Juzi Novemba 20, 2019 akizungumza na wananchi wa Gairo
Mkoani Morogoro wakati akiwa safarini kuelekea Jijini Dodoma Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliwataka wakulima na wafanyabiashara
kupandisha bei ya mahindi kutokana na hali ya soko huku akisisitiza kuwa
serikali anayoiongoza haitopanga bei elekezi ya mahindi.
Alisema serikali anayoiongoza haiwezi kupanga bei elekezi
ya mahindi kwani kufanya hivyo itakuwa imefilisika kiutawala, hivyo mahindi
yatajiendesha kulingana na soko kwani huu ni mwaka wa wakulima hivyo wapandishe
tu bei kadri wawezavyo kulingana na soko.
Mhe Rais alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa kwa
mwananchi yeyote atakayeona mahindi yamekuwa ya bei ya juu aende akalime ya bei
ya chini.
Aidha, Waziri wa Kilimo amesema kuwa serikali ya awamu
ya tano imejipanga kumkomboa mkulima ili kunufaika na jasho lake hivyo imnaendelea
kuimarisha kitengo cha masoko ikiwa ni mkakati maalumu wa kuhakikisha kuwa
wakulima wanajipatia kipato kizuri kwa kuwa na soko la uhakika la bidhaa za
kilimo ndani na nje ya nchi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment