Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani), kuhusu tathimini ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (Pichani), kuhusu tathimini ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019), Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari wakitekeleza majukumu yao katika Mkutano wa Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, kuhusu miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano chini Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Novemba 6, 2019), Jijini Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).
***********************************
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
6.11.2019
SERIKALI imesema imeweka mifumo
imara ya kitaasisi na kisheria inayohakikiwa kuwa miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na itakayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano
inaendelea kuleta manufaa endelevu kwa faida ya Watanzania wote.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano wake na Waandishi wa
Vyombo vya Habari aliozungumzia kuhusiana na tathimini ya miaka minne ya
Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli.
Dkt. Abbasi alisema yapo mambo
mengi na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na itakayotekelezwa
na Serikali ya Awamu hivyo ili kuwezesha mafanikio yake yanaleta matokeo
chanya kwa Watanzania na jamii kwa ujumla, Serikali imeweka mifumo
imara ya kitaasisi na kisheria kwa ajili ya kulinda mafanikio hayo hata
baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kumaliza muda wake.
‘‘Tanzania kwa sasa ndani ya
kipindi kifupi cha miaka minne ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano
tumeweza kufanya mambo mengi ikiwemo suala la rushwa ambalo limekuwa
kero kubwa kwa Watanzania na hilo kwa sasa tumeunda Mahakama maalum ya
Mafisadi ambayo tayari imesikiliza kesi zaidi ya 50’’ alisema Dkt.
Abbasi.
Aidha aliongeza zipo ahadi za
utelezaji wa miradi na mipango mbalimbali ya Serikali iliyoahidiwa
kufanywa na Rais Dkt. John Magufuli ambayo awali ilikuwa ikileta kero na
kuchelewesha maendeleo ya Watanzania, ambapo ndani ya kipindi kifupi
cha miaka minne ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano yameweza
kutekelezwa.
Akifafanua zaidi Dkt. Abbasi
alisema ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. John
Magufuli, Serikali ya Awamu ya Tano imeweza kutimiza ahadi mbalimbali
ambazo tayari zimeanza kuleta matokeo chanya kwa Watanzania ikiwemo
ununuzi wa ndege za Serikali ambapo awali jambo hilo lilikuwa na ugumu
katika utekezaji wake.
‘Jambo jingine ni suala la
kuhamia Dodoma, jambo hili kwa sasa si ndoto tena kwani kwa sasa
asilimia 90 ya watumishi wa Serikali katika Wizara na baadhi ya Idara,
Taasisi na Wakala za Serikali wamehamia Dodoma na Serikali imeweza
msingi wa kisheria wa kuitangaza Dodoma kuwa ni makao makuu ya
Serikali’’ alisema Dkt. Abbasi.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema
ili maendeleo hayo yazidi kuleta manufaa endelevu kwa vizazi vijavyo,
Watanzania hawana budi kuwa wazalendo na kuwa walinzi wa mali za umma na
kutoa taarifa katika mamlaka za serikali kuhusu uharibifu na ubadhirifu
unaofanywa na mtu au kikundi chochote katika jamii.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema
Serikali ya Awamu ya Tano kupitia ushirikiano wake na wananchi imeweza
kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo
ujenzi wa vituo vya afya, maji, elimu na barabara, ambayo imeendelea
kuwagusa wananchi wengi zaidi hususani wa kipato cha chini.
Akitolea mfano, Dkt. Abbasi
alisema Serikali inatekeleza miradi ya maji 1600 nchi nzima ikiwemo
miradi 300 inayotekelezwa katika maeneo ya vijijini na kutumia kiasi cha
Tsh Bilioni 700 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo katika maeneo ya
mijini ili kuhakikisha kuwa inafikia kiwango cha asilimia 85 vijijini na
asilimia 95 maeneo ya mijini ifikapo mwaka 2020.
Kuhusu sekta ya afya, Dkt. Abbasi
alisema Serikali kwa sasa imeendelea kuimarisha sekta hiyo kwani kwa
sasa Tanzania imekuwa nchi mfadhili kwa kuweza kufanya huduma mbalimbali
za kibingwa ambazo zilikuwa zikifanyika nje ya nchi na kuifanya
Serikali kupoteza kiasi kikubwa cha fedha za Watanzania.
‘Ndani ya kipindi cha miaka minne
Serikali imeweza kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Tsh
Bilioni 31 mwaka 2014/15 hadi kufikia Bilioni 270, na pia kuajiri
waganga wataalamu zaidi ya 6000 wanaohudumia wagonjwa katika hospitali
zetu za Mikoa, Wilaya, Vituo vya Afya katika Kata na Zahanati katika
maeneo ya vijijini’’ alisema Dkt. Abbasi.
0 comments:
Post a Comment