***********
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Joseph
Buchweishaija amewataka watanzania wote kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika maadhimisho na maonyesho ya nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuia ya
Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) Maadhimisho na Maonesho hayo
yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Agosti 2019 katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC); Viwanja vya Karimjee
na Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Profesa Bucheishaija amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya
Viwanda na Biashara inawaalika wananchi kufika kwa wingi kwani
tunatarajia jumla ya nchi 15 wanachama wa SADC zitashiriki.
Aidha, ameongeza kuwa wiki hii ya SADC itawawezesha wananchi
kuona fursa mbalimbali ikiwemo kuweza kupata malighafi za kilimo ambazo
viwanda utumia kuzalisha bidhaa za viwandani. Miongoni mwa faida
watakazozipata watanzania kupitia maonesho ya Viwanda kwa nchi za Kusini
mwa Afrika ni pamoja na kujifunza au kubadilishana uzoefu na nchi
nyingine za SADC ambazo zitashiriki katika maonesho hayo pamoja na
kuongeza wigo wa masoko ya ndani na nje ya nchi. Nafasi imetolewa kwa
kila mtanzania kujisajiri bado ipo mpaka tarehe 2 August, 2019 na wale
ambao watakuwa hawajajisajiri wasiwe na wasiwasi maana nao watatembelea
maeneo ya maonesho kama wengine na kuweza kuona bidhaa za nchi nyinyine,
hivyo watu wote wanakaribishwa sana kwa ajili ya tukio la kihistoria
ambalo kutokea tena mpaka ipite miaka kumi na mitano.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda na Biashara ndugu Ludovick Nduhiye ametoa ufafanuzi kuwa lengo
kuu ni kuweka utayari kwa wananchi hususani kwa Tanzania kuweza
kushiriki kwa wingi na kuweza kujionea fursa lukuki ambazo zitaonekana
katika maoshesho hayo.
Aidha bwana Nduhiye amewakaribisha wananchi kufika kwa wingi
lengo likiwa ni kuangailia fursa muhimu zitakazopatikana kwenye wiki
hiyo ya viwanda ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko pamoja na
ubadilishaji wa mawazo namna ya kuanzisha viwanda mbalimbali pamoja na
kupata fursa mbalimbali kwenye nchi hizo za SADC. Naye mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya maonesho na maadhimisho ya Wiki ya Viwanda
kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara bwana Ally Gugu ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya Mtengamano na Biashara amewahimiza wananchi
kujisajili kupitia anuani zinazopatikana katika tovuti ya Wizara ya
Viwanda na Biashara ambayo ni www.mit.go.tz na kisha kubofya katika
linki mbili za haraka (quick link) ambazo ni Usajili Wiki ya Viwanda na
Usajili Mkutano wa 39 wa SADC.
Gugu aliongezea kuwa haya maonesho ya viwanda ni fursa ya
watanzania wote kuanzia wajasiriamali wadogo, wajasiriamali wa kati
pamoja na wenye viwanda vikubwa ili tuweze kutimiza azima ya Serikali ya
awamu ya tano inayosisitiza maendeleo kupitia uchumi wa Viwanda ili
Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati.
0 comments:
Post a Comment