Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi na Wafanyakazi wa Shamba la
China State Farms lililopo Wilaya ya Kilosa alipofanya ziara ya
kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoa wa Morogoro, Julai 31, 2019.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa shamba la China State Farms wakimsikiliza kwa makini
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani)
alipotembelea shamba la China State Farms lililopo Wilayani Kilosa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kutokea kulia) akisikiliza kero kutoka
kwa mmoja wa wafanyakazi wa Shamba hilo Bw. Azory Andrea kuhusu mikataba
inayotolewa na mwekezaji wa shamba hilo.
Kamishina Msaidizi wa Kazi, Bi.
Rehema Moyo akitoa ufafanuzi kuhusu mkataba wa kazi wa Bw. Azory Andrea
(hayupo pichani) alipowasilisha tatizo lake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea hilo la China State Farms,
Wilayani Kilosa Julai 31, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiangaalia katani iliyoanikwa, wakati
alipotembelea shamba hilo lililopo wilayani Kilosa. Kushoto anayetoa
maelekezo ni Meneja wa Rasilimali watu na Fedha Bw. Athumani Migeto.
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Meneja Rasilimali Watu wa
Shamba la China State Farms Bw. Athumani Migeto (kulia) alipotembelea
sehemu ya mitambo ya uzalishaji. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa
Mhe. Adam Mgoyi.
Muonekano wa Nyumba zilizojengwa na Uongozi wa Shamba la China State Farms kwa ajili ya wafanyakazi wa shamba hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na wawekezaji wa Shamba la Katani la
China State Farms lililopo Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt.
Steven Kebwe akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama alipomtembelea katika ofisi yake Julai 31, 2019 kabla ya
kutembelea maeneo ya kazi yaliyopo katika Mkoa huo.
***********
Hayo ameyasema na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Shamba la Katani la
China State Farms lililopo wilayani Kilosa ikiwa ni ziara yake ya
kutembelea maeneo ya kazi.
Akizungumza mara baada ya kuwasili
katika shamba hilo alieleza kuwa wawekezaji wakiwa kama waajiri lazima
wahakikishe wanafuata sheria za kazi katika maeneo yao ya uzalishaji
kwa kuzingatia masuala ya msingi ya wafanyakazi ili waweze kuzalisha kwa
tija na kuwahamasisha kufanya kazi zao kwa juhudi.
“Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeendelea
kuboresha mazingira ya biashara ambayo yamekua yakivutia zaidi
wawekezaji, hivyo sera nzuri zilizopo nchini zimekuwa chachu kwa
wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu,” alisema Mhagama
Alieleza pia, endapo wawekezaji
watafuata miongozo ya kisheria katika masuala ya kazi na ajira
yatawarahisishia utendaji wao wa kazi.
Akitolea mfano kuhusu masuala ya
kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi, likizo ya uzazi kwa wanawake, uwazi wa
mikataba ya ajira, uhuru wa mfanyakazi kujiunga na chama cha
wafanyakazi, haki ya kupatiwa vitendea kazi na maslahi ya wafanyakazi ni
baadhi ya vitu vya msingi ambavyo mwekezaji inabidi atoe kwa mfanyakazi
wake kwa kuzingatia taratibu na sheria.
Hata hivyo aliongezea kuwa
ushirikiano na vyama vya wafanyakazi ni jambo la muhimu kwa kuwa
vimekuwa vikitetea masuala ya wafanyakazi ambayo yamekuwa yakijitokeza
katika maeneo yao ya kazi, pamoja na kuwa na mkataba wa hali bora za
wafanyakazi baina ya mwajiri na mwajiriwa.
Sambamba na hilo Mheshimiwa
Mhagama alitoa maagizo kwa timu ya wataalamu ambao aliambatana nayo
kutoka Idara ya Kazi, Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA),
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF), Tume ya Usuluhisi na Uamuzi pamoja na Viongozi wa
vyama vya Wafanyakazi kuendelea kutoa elimu kwa umma hususan wafanyakazi
ili watambue sheria za kazi na namna taasisi hizo zinaweza kuwasaidia
katika kupata ufumbuzi wa masuala yao ya kazi.
Aidha, Waziri Mhagama alitoa
pongezi vilevile kwa wawekezaji wa Shamba la Katani la China State Farms
kwa kuwajali wafanyakazi wao ikiwa na kuwajengea nyumba bora za kuishi
wafanyakazi wao.
“Nimpongeze mwekezaji kwa kuona
umuhimu wa kuwajengea makazi wafanyakazi ambayo yatamaliza kabisa tatizo
la upatikanaji wa nyumba na umbali ambao wafanyakazi wamekua wakitumia
kwenda kazini,” alisema Mhagama
Pia, alitumi muda huo
kuwahamasisha wafanyakazi kutumia muda wao wa ziada katika mashamba yao
binafsi na kujiunga kwenye mashamba ya ushirika yatakayo wawezesha
kupata soko la uhakika kutoka kwa mwekezaji huyo ili waweze kuimarika
kiuchumi.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa
Mhe. Adam Mgoyi alisema kuwa Sheria za kazi zimekuwa zikitoa mwongozo
mzuri kwa wawekezaji katika kuimarisha shughuli zao za uzalishaji, kutoa
ajira pamoja na kuchangia kwenye mapato ya nchi.
Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda
hicho Bw. Majuto Chitema alitoa pongezi zake kwa Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kusifu juhudi alizonazo katika kuboresha na
kuwajengea mazingira wezeshi wawekezaji, kwani serikali yake imeweza
mstari wa mbele kuweka sera, miongozo, kanuni na sheria ambazo zimekuwa
haziwabani wawekezaji.
Miongoni mwa Wafanyakazi wa China
Estate Farms Bw. Azory Andrea alisema kuwa Serikali iendelee kuangalia
namna ya kuwa kuwasimamia wawekezaji waliopo nchini ili waweze
kutekeleza wajibu wao kwa wafanyakazi kwa mujibu wa sheria za kazi.
Kabla ya ziara hiyo Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwasili katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata taarifa ya maeneo
aliyoandaliwa kutembelea katika ziara yake mkoani hapo.
0 comments:
Post a Comment