Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson ametunukiwa Uanachama wa maisha na Shirika la
Msalaba Mwekundu nchini (Tanzania Red Cross).
Dkt Tulia ametunukiwa uanachama huo leo tarehe 6 Octoba
2019 katika Mkutano wa Taifa wa Shirika hilo uliofanyika Jijini Dodoma baada ya
kukubali kuwa Balozi.
Dkt. Tulia amesema “Niwashukuru kwa ombi hili zito
mlilonipa na nilipokee kwa unyenyekevu kabisa kwa kusema kwamba nimekubali kuwa
balozi wa kudumu na nitafanya kazi hiyo kwa uaminifu kabisa”
“Niwatakie kila la kheri Viongozi wote na Wanachama wa
Red Cross, Wakati sisi tunakua ilikuwa tukiliona gari la Red cross tulikuwa
tunakimbia mbio kwa sababu ilikuwa inaonekana kana kwamba ni wanyonya damu,
lakini mambo haya yameisha kwenye jamii kwasababu ya kazi kubwa na nzuri
mnayoifanya kwa jamii ikiwemo kutoa elimu na watu wamefahamu kwamba nyie sio
wanyonya damu bali ni watoa huduma za kibinadamu” Alisema Dkt. Tulia
0 comments:
Post a Comment