Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimpokea Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alipowasili Mkoani humo
kwa ziara ya siku moja
Waziri Bashungwa akiweka bayana kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lengo la ziara yake alipomtembelea ofisini kwake.
Waziri wa Viwanda Mhe. Innocent Bashungwa
pamoja na mwenyeji wake Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro wakipokelewa na wenyeji wao katika kiwanda cha nguo cha 21C.
cha Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya siku moja Juni 29 mwaka huu.
Kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21st Centuary cha Mkoani Morogoro kinavyoonekana kwa ndani
………………………….
Na. Andrew Chimesela – Morogoro
Waziri wa Viwanda na Biashara hapa nchini
Innocent Bashungwa amezitaka taasisi za SIDO, TIRDO, CAMATEC na TEMDO’S
kuamka kutoka usingizini na kujikita katika kuandaa vijana na akinamama
kupata ujuzi mbalimbali ili waweze kuajiriwa viwandani ikiwa ni sehemu
ya kutatua changamoto kubwa iliyojitokeza wakati anatembelea viwanda
Mkoani Morogoro.
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wakati
wa ziar yake ya siku moja Mkoani Morogoro ikiwa na lengo la kutembelea
viwanda vya kuchakata mazao ya wakulima ikiwemo kiwanda cha nguo cha 21st
Centuary, kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava, na
kiwanda cha Tumbaku cha TTPL ambavyo vyote viko katika Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro.
Waziri Bashungwa amesema taasisi hizo za
SIDO TIRDO, CAMATEC na TEMDO’S ambazo ziko chini ya Wizara yake
ziliazishwa mahususi kwa ajili ya kutatua changamoto kama hizo
zinazojitokeza viwandani na kuzitaka taasisi hizo kujikita katika kutoa
ujuzi kwa Vijana na akinamama hasa ujuzi unaohitajika na viwanda hivyo
ili waweze kuajiriwa huku akizitaka mamlaka hizo kwenda katika viwanda
alivyotembelea ili kukaa pamoja na kutengeneza program zitakazofanikisha
kuondoa changamoto hiyo.
“Mtaani wanatafuta ajira huku
viwandani wanasema tunataka vijana wenye ujuzi wa namna hii na mimi ni
Waziri wa Viwanda na Biashara, kwa hiyo nimeagiza SIDO, TIRDO, CAMATEC, na TEMDO’S ambao wako chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara waamke kutoka usingizini” amesema Waziri Bashungwa.
Agizo hilo limekuja baada ya Waziri
Bashungwa kupokea changamoto ya aina moja kwa viwanda viwili kati ya
vile alivyovitembelea kikiwemo kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21st
Centuary na kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava vya
Mkoani Morogoro huku wamiliki wa viwanda hivyo wakilalamika kutumia muda
mrefu kuwafundisha vijana hadi kufanikiwa kufanya kazi kwa ufanisi
kiwandani.
na kusababisha Waziri kuagiza mamlaka
hizo kufika katika viwanda alivyotembelea ili waweze kukaa pamoja na
kutengeneza program zitakazofanikisha kuondoa changamoto hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa
amesema ni azma yake kutaka atatembelea viwanda vyote vya hapa nchini
vinavyochakata mazao ya wakulima (Textile Industries)
ili kujua changamoto zake na kuzitatua ili viwanda hivyo viweze
kutimiza azma ya Serikali ya wakulima wa mazao ya pamba na tumbaku
kupata bei nzuri na masoko ya uhakika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambaye aliambatana na Waziri huyo wakati wa
ziara hiyo alizungumzia zaidi ufanisi na changamoto za Kiwanda cha
tumbaku cha TTPL ambapo pamoja na kukiri kuwa Kiwanda kinafanya vizuri
lakini ameiomba Serikari kuendelea na mazungumzo ili kutatua changamoto
iliyopo kiwandani hapo ambayo tayari imeripotiwa ngazi ya Wizara.
Kwa upande wao wamiliki wa viwanda vya
21st Centuary na kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava
kupitia risala iliyosomwa na meneja msaidzi wa Kiwanda cha Mazava Bw.
Nelson Mchupya wamesema pamoja na mafanikio yaliyopo bado
wanachangamoto, kubwa ni ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi kwa kazi
wanazotakiwa kuzifanya kiwandani hapo.
Huku Kiwanda cha Mazava kilichoazishwa
mwaka 2018 na kujihusisha na kutengeneza nguo za michezo ambazo kinauzwa
nchini Maerekani kwa asilimia mia kilianza na wafanyakazi 300 huku
kikisafirisha kontena 40 za futi 40 sawa na wastani wa nguo laki moja
kwa mwezi, kwa sasa kiwanda kimeajiri wafanyakazi 2,161 na kinasafirisha
makontena 16 ya futi 40 sawa na nguo milioni moja kwa mwezi
zinasafirishwa nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment