![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/CU3a1957.jpg)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Tombe Magufuli akiongea kwa simu na Mkuu wa Jeshi la
Polisi IGP Simon Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi mara moja Mkuu wa
Polisi wa Wilaya ya Sumbawanga ACP Polycarp Urio kwa kutowasilisha
taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa maelekezo ya Waziri wa
Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola ambaye hivi karibuni aliagiza
kuhamishwa kituo cha kazi askari polisi Tisa waliokuwa wakijihusisha na
vitendo vya rushwa na kuwabambikizia kesi wananchi. Mhe. Rais alitoa
matatizo hayo alipotembelea Kituo cha Polisi cha Laela mara baada ya
kuzindua rasmi Barabara ya Tunduma-Laela-Sumbawanga yenye urefu wa
kilometa 223.2
ambayo ni sehemu ya barabara kuu katika ushoroba wa Magharibi
unaoanzia Tunduma-Mpanda-Kigoma-Nyakanazi wenye urefu wa kilometa
1,286.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment