Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt.Ayoub Rioba akitoa semina kwa wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu umuhimu wa shirika hilo kuzingatia maudhui ya kitanzania zaidi badala ya mudhui ya mataifa mengine leo jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuanzisha matumizi ya teknolojia ya matumizi ya ‘CAM’.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Peter Serukamba
akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuzingatia ubora katika uandaaji wa Makala za Chaneli ya Utalii ya SAFARI wakati wa Semina ya wabunge wa kamati hiyo (hawapo pichani) leo Jijini Dodoma,kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Juma Nkamia (katikati) akitoa angalizo kwa uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kufuatilia maudhui ya redio za jamii kwani nyingi zimekuwa na changamoto ya maudhui wakati wa semina Semina ya kuwajengea uwezo wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuleta mfumo wa matumizi ya ‘’CAM’’ kwa televisheni iliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Leseni Mhandisi Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya Mawaliano Tanzania akitoa semina kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuleta mfumo wa matumizi ya ‘’CAM’’ kwa televisheni ambapo mteja hata lazimika kununua kisimbusi zaidi ya kimoja ilikupata kifurushi bali atanunua kifaa hicho na kukiweka katika kisimbusi aina yoyote.
*****************************
Anitha Jonas – WHUSM
12/09/2019
Dodoma.
Serikali ya ahidi kuendelea kuboresha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa
kuhakikisha linakuwa na muonekano bora kama mashirika ya Kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa Semina ya
kuwajengea uwezo wabunge kuhusu mpango wa serikali wa kuboresha mfumo wa Visimbusi kwa kutaka kuanzisha utaratibu wa kununua kifaa maalum kitakachobeba kifurushi ambacho kinaitwa ‘’CAM’ kifaa hicho kitatumika badala ya kununua zaidi ya kisimbusi kimoja.Semina hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
‘’Na serikali inampango endelevu wa kuboresha TBC na kuifanya ya kisasa zaidi na ndiyo maana tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imekuwa ikiongeza Bajeti ya Maendeleo kwa Shirika hilo na lengo ni kuifanya iwe yenye bora zaidi,’’alisema Shonza.
Akiendelea kuzungumza katika Semina hiyo Mheshimiwa Shonza alitoa wito kwa
wanasiasa wote wa vyama vya upinzani kujitokeza na kukitumia chombo cha TBC
kwani shirika hilo ni la umma na halina ubaguzi kwa wanachama wa upinzani kama inavyosemekana kwani linaendeshwa kwa kodi za wananchi.
Kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Huduma na Maeneleo ya Jamii
Mhe.Peter Serukamba alitoa rai kwa uongozi wa TBC kuhakikisha unatumia wapiga picha wenye weledi wakati wa uandaaji wa Makala za utalii kwa ajili ya Chaneli ya Utalii ya TANZANIA SAFARI CHANELI kama chaneli nyingine za wadau wa utalii.
Halikadhalika nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii Mhe.Juma Nkamia alitoa angalizo kwa uongozi wa TCRA kufuatilia kwa
umakini Maudhui ya Redio za Kijamii kwani redio hizo zisipofuatiliwa kwa karibu
zinaweza kuleta changamoto hivyo ni vyema waweke mkakati madhubuti wa
kufuatilia vituo hivyo.
0 comments:
Post a Comment