Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) wakifatilia hotuba ya mhgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019.
Katibu Mkuu wa Wiziri ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa taarifa ya Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) wakati wa hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali
imesema kuwa imekusudia kuimarisha utoshelevu wa chakula nchini, ili kuchangia
utoshelevu wa chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo
ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC), na kuwa kinara wa soko la mchele katika Jumuiya za Kikanda.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
ameyasema hayo tarehe 16 Disemba 2019 wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza
Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma.
Ili
kufikia azma hiyo, Waziri Hasunga amesema kuwa serikali imeweka kipaumbele
katika malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora za mpunga ambazo
zinastahimili ukame na kuhamasisha matumizi ya teknolojia bora za uzalishaji
zitakazo himili mabadiliko ya tabia nchi na Kupunguza gharama za uzalishaji na
kuweka mifumo bora ya udhibiti ili mchele wetu uweze kushindana kwa bei na
ubora na michele inayotoka nje ya nchi.
Malengo mengine ni Kuimarisha mifumo ya uzalishaji na masoko
hususani kwa wakulima wadogo ili kukifanya kilimo cha zao la mpunga kuwa
endelevu na kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi; na Kuongeza eneo la kulima
zao la mpunga katika maeneo ya umwagiliaji na yanayotegemea mvua.
Pamoja na mikakati hiyo muhimu kabisa ya kuimarisha zao la mpunga Pia
amesema kuwa serikali imekusudia kuimarisha na kuboresha miundombinu ya
umwagiliaji na kuwajengea uwezo wakulima kuhusu usimamizi wa miundo mbinu hiyo.
Ili kufikia malengo hayo Waziri Hasunga amesema
kuwa Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na wadau wa zao la Mpunga nchini itahakikisha
inasimamia inaongeza eneo
la uzalishaji wa mpunga kutoka hekta milioni 1.1 za mwaka 2018 hadi hekta
milioni 2.2 ifikapo mwaka 2030;
Kuongeza tija ya
uzalishaji wa mpunga kutoka wastani wa tani 2.2 kwa hekta hadi kufikia wastani wa tani 4.4 kwa hekta
ifikapo mwaka 2030; Kuimarisha kilimo
cha umwagiliaji na kuhamasisha teknolojia za umwagiliaji zinazotumia maji kwa ufanisi na Kuongeza thamani ya zao la mpunga kutoka asilimia
10 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2030 ikiwa ni pamoja na kupunguza upotevu kabla na baada ya mavuno.
Kadhalika kuimarisha mifumo ya masoko na kilimo biashara; Kuongeza upatikanaji wa mbegu bora za mpunga pamoja
na kuimarisha mifumo ya mbegu; Kuongeza upatikanaji wa mbolea kwa kuanzisha
Viwanda vya kuzalisha na kuchanganya mbolea nchini ikiwa ni pamoja na mifumo ya
masoko na usambazaji; na Kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza
thamani na kuboresha mifumo ya masoko na upatikanaji wa mitaji.
Waziri Hasunga amnetumia mkutano huo kuyasihi
makampuni ya kimataifa ya JICA, HELVETAS, IRRI, RIKOLTO, BRiTEN, AGRICOM na Wadau
wengine kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Mkakati huo ambao
umeainisha viashiria chanya vya kuendeleza zao la mpunga; na hatimaye kuifanya nchi
kuwa mzalishaji na soko kuu la mchele katika ukanda wa Afrika Mashariki na
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika.
Alisema kuwa pamoja
na kukamilika kwa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mkakati wa Kuendeleza Zao
la Mpunga (NRDS I) na kuonesha mafanikio makubwa, ni dhahiri kuwa bado kunahitajika
kuongeza tija na uzalishaji zaidi. Hivyo hiyo ndio sababu iliyopelekea Wizara
ya Kilimo kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo kuandaa Mkakati wa Kuendeleza
Zao la Mpunga Awamu ya Pili (National
Rice Development Strategy Phase II - NRDS II) utakaotekelezwa kwa kipindi
cha miaka kumi (10) kuanzia Mwaka 2019/20 hadi Mwaka 2029/30.
Lengo kuu la Mkakati huo ni kuongeza uzalishaji
wa zao la mpunga, kuimarisha usalama wa chakula na lishe, pato la wakulima na
Taifa kwa ujumla ifikapo Mwaka 2030.
Ameongeza kuwa Uandaaji wa Mkakati huo ni
matokeo ya Mkutano Mkuu wa Coaliation for African Rice Development (CARD) uliofanyika
Jijini Tokyo, Japani Mwezi Oktoba, 2018 ambao ulikuwa na malengo makuu mawili
ambayo ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa CARD awamu ya kwanza kipindi cha
mwaka 2008 hadi 2018 na kuona namna gani awamu ya pili ya Mkakati huo itakavyotekelezwa
kwa kipindi cha Mwaka 2019 hadi 2030.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment