Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imekiagiza Chama cha
Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education -
TSAEE) kutumika kama chombo cha kuishauri Serikali katika kuboresha utoaji wa
huduma za ugani hapa nchini pamoja na kuwa ni kiungo cha kuwaunganisha watoa
huduma za ugani na wadau mbalimbali hapa Nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) ametoa kauli hiyo tarehe 16 Disemba 2019 wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama
cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education -
TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma.
Amekitaka chama hicho kusimamia weledi wa Maafisa
ugani katika kutekeleza majukumu yao; pia kwa lengo la kuimarisha uhai wa chama
amewataka wajumbe wa chama hicho kukutana mara kwa mara ili kujadili mafanikio
na changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za ugani nchini na kutoa ushauri
kwa Serikali namna ya kutatua changamoto hizo.
Pia amewataka Wajumbe, kwa kushirikiana na Viongozi
wa Chama hicho kuongeza ubunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato kwa ajili ya
kuimarisha na kuendesha Chama huku akiwasisitiza kuwa wakati wa uchaguzi wahakikishe
wanachagua viongozi makini watakao simamia na kuongoza Chama hicho ili kiwe
imara na endelevu.
Kwa upande wa Maafisa Ugani, ili kuweza kuimarisha utendaji wa
majukumu yao ya kila siku na hatimaye kuinua sekta ya kilimo nchini, Waziri Hasunga
ameagiza kila Afisa Ugani kuwa na Daftari la Kilimo ambalo atalitumia kuweka
kumbukumbu zote za muhimu kila atakapoenda kuwahudumia Wakulima.
Amesema kuwa pamoja na
taarifa nyingine za msingi, Daftari hilo lioneshe orodha ya wakulima
anaowahudumia, ukubwa wa mashamba yao na aina ya mazao wanayolima.
Ameongeza kuwa Afisa Ugani ni lazima awe na
Mpango kazi utakaoonesha ni nini hasa amepanga kufanya kwa wakulima, ikiwa ni
pamoja na kuainisha ratiba ya kazi kwa kipindi husika huku akitaka kila Afisa
Ugani kuwa na mashamba ya mfano au mashamba darasa ambayo atayatumia
kuwafundishia Wakulima katika Kata/Kijiji/Mtaa wake.
Kadhalika ameagiza kuwa Afisa Ugani ni lazima
awe na Mwongozo wa kusimamia Huduma za ugani na kuhakikisha anausimamia
ipasavyo pamoja na kufahamu kanuni au mbinu bora za kilimo cha mazao makuu yote
yanayolimwa katika eneo lake.
Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itaendelea
kushughulikia changamoto kwa kutoa msukumo wa kutosha kwa ajili ya uendelezaji
wa sekta hizo muhimu hususani kupitia Utekelezaji wa Programu mbalimbali
ikiwemo Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).
Aidha, Amesema kuwa serikali pia
itaendelea kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi ambao
wanaonesha dhamira ya dhati ya kuungana na serikali katika kuhakikisha Tanzania
inafikia uchumi wa kati kupitia shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment