Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe
Na Innocent Natai, TPRI, Arusha
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameshangazwa na kuwepo kwa baadhi ya
halmashauri zinazotoza ushuru wa mazao ya mbegu,kitendo ambacho ni kinyume na
maelekezo ya serikali na kinarudisha nyuma jitihada za serikali za kuhakikisha
nchi inaongeza uzalishaji wa mbegu na kuacha kununua mbegu kutoka nje ya nchi.
Mtigumwe ameyasema hayo tarehe 17 Disemba 2019
wakati wa kikao cha utekelezaji wa tasnia ya mbegu hapa Nchini, ikiwemo
kupitisha aina mpya za mbegu bora za mazao, kupitia changamoto za uzalishaji wa
mbegu hapa nchini, Kilicho jumuisha ujumbe kutoka TARI (Tanzania
Agricultural Research Institute), Ofisi ya hatimiliki za wagunduzi wa mbegu,
Idara ya mazao, na Taasisi ya udhibiti ubora wa mbegu (TOSCI).
Wengine ni Chama cha
Wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania, Mwakilishi kutoka
Vyuo vikuu vya Kilimo, Maendeleo ya Mazao, Mtandao wa Vikundi
vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), na Wakala wa mbegu za
kilimo (ASA) uliofanyikia katika ukumbi wa mikutano TPRI Makao Makuu
Arusha.
Amesema halmashauri kutoza ushuru kwenye mazao ya
mbegu ni kosa kwani maelekezo ya serikali kuhusu suala hilo yalishatolewa na mbegu
za kilimo ni tofauti na mzao ya chakula na biashara yanayo zalishwa, hivyo
kufanya hivyo kunakwamisha adhma ya serikali ya kuhakikisha uzalishaji wa mbegu
unaongezeka na taifa kuacha kununua mbegu kutoka nje.
Amesema serikali imejipanga kuhakikisha suala hilo
linafanikiwa kwa kipindi kifupi ikiwemo kuwaondolea vikwazo wazalishaji wa
mbegu na kuwatatulia kero mbalimbali zinazowafanya washindwe kuzalisha kwa
wingi na kuwataka wazalishaji wa mbegu kutoa nje kufanyia uzalishaji wa
mbegu zao hapa nchini na kuacha ule utaratibu wa awali wa kuzalishia nje na
kuja kuuza hapa nchini.
Aidha, amezitaka taasisi zote zinazohusiana na
tasnia ya Mbegu kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ili kusaidia mkakati wa
kitaifa wa uzalishaji mbegu unatimia ikiwemo kuhakikisha wanatoa elimu
kwa wakulima ya kutambua mbegu bora,mbegu zisizo bora,kanuni za mbegu bora
ikiwemo kuacha kurudia mbegu kwa muda mrefu.
Ameitaka Taasisi ya Kudhiti Ubora wa
Mbegu (TOSC) kuhakikisha inaongeza kasi ya ukaguzi na kubaini wauzaji na wasambazaji
wa mbegu zisizo bora na feki au bandia na watakao bainika kuchukuliwa hatua ili
kuwahakikishi wakulima usalama wa kilimo chao na kufanya tasnia ya kukua
na taifa kujitosheleza kwa mbegu zilizo bora.
Kakao hicho kimeazimia kwa pamoja kupitisha aina
mpya za mbegu bora za mazao takribani 40 ambazo ni za mazao ya Mahindi aina 10,
Mpunga aina 2, Ulezi aina 1, Pamba aina 3, Mhogo aina 9, Alizeti aina 9 na
Viazi vitamu aina 6.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment