METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, December 14, 2019

MKAKATI WA KUENDELEZA ZAO LA MPUNGA AWAMU YA PILI: 2019-2030 KUZINDULIWA DISEMBA 16-MHANDISI MTIGUMWE


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew J. Mtigumwe

Dodoma 14 Desemba, 2019

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewajulisha  wananchi na wadau wa kilimo nchini kuhusu kufanyika kwa uzinduzi wa Mkakati wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (National Rice Development Strategy Phase II).

Mkakati huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi (10) kuanzia mwaka 2019/2020 hadi mwaka 2029/2030. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 16 Desemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa St. Gaspar Jijini Dodoma kuanzia saa 2.00 asubuhi.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo atakuwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb). Wadau wa zao la mpunga na wananchi wanaalikwa kuhudhuria kwenye uzinduzi huo.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com