Leo Septemba 20, 2019 Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya kutangaza Utalii Nyanda za Juu
Kusini.
Maadhimisho hayo yenye kauli
mbiu ijulikanayo kama "Karibu Kusini kwa Utalii na Uwekezaji" yanafanyika
katika Viwanja vya Kihesa Kilolo Mkoani Iringa kwa siku tatu mfululizo.
Akitoa hotuba yake Dkt Tulia
amewasihi viongozi na wadau mbalimbali wa Mikoa ya Kusini kuwa wabunifu zaidi
katika kubuni na kuibua vivutio ambavyo vinajitofautisha na maeneo mengine na
havipatikani mahali popote pale isipokuwa katika Mikoa hiyo.
“Ni wazi kuwa Utalii ni moja
ya sekta inayochangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa hivyo huu ni wakati wetu
kuwekeza na kuboresha sekta hii” Alisema
0 comments:
Post a Comment