Wajumbe
wa mkutano wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo IV Uliopo wizara ya
kilimo mkoani Dodoma mara baada ya wasilisho la mfumo wa AfriFarm
wakichangia maoni yao katika kuboresha mfuo huo uliofanyika hivi karibuni
Na
Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Shirika la Kimarekani
linalojihusisha na miradi mbalimbali ya kilimo na elimu (project concern international)
PCI leo wamewasilisha matokeo ya matumizi
ya mfumo wa Afrifarm katika kupambana na kiwavijeshi vamizi fall armyworms katika mkutano uliofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa Kilimo IV Uliopo
Dodoma na kuhusisha wataalamu mbalimbali na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Kilimo
.
Mfumo huo ambao hutumika
Zaidi kwenye simu ganja uliogunduliwa na Shirila la PCI kwa lengo la kupambana na kiwavijeshi vyamizi katika Mkoa wa Mara ikihusisha
kutoa mafunzo ya utambuzi wa kiwavijeshi vamizi (FAW identification) ,ukaguzi wa mashamba, FAW field scouting na kutoa taarifa za kiwango cha mashambulizi katika
ngazi ya jamii husika
Akiongea wakati
wa ufunguzi wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya kilimo ambaye ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango
sehemu ya Ukusanyaji wa Taqwimu Bwana… ..Rubboa amesema shirika hilo kwa kushirikiana
na Kitengo cha Huduma ya Afya ya Mimea (PHS) chini ya Wizara ya Kilimo, Kampuni
ya Dimag walifikia hatua kubwa ya kuvumbua mfumo huo wakielekitroniki unaoitwa AfriFARM,
(Africa fall armyworm Response Mechanism).
Akiuelezea mfumo huo
Bwana Luboa amesema kwamba AfriFARM ni mfumo wa simu (mobile phone application) uliobuniwa ili kumuwezesha Afisa ugani au mkulima kujifunza juu ya ufahamu wa kiwavijeshi vamizi, ukaguzi wa shamba na mbinu mbalimbali
za kukabiliana na uvamizi huo.
Aidha shirika la
PCI limewekeza katika kukuza matumizi ya
teknolojia ambapo lilifanya majaribio katika Kata 45 zilizoko katika wilaya ya Butiama, Bunda na
Musoma vijijni katika Mkoa wa Mara ambako kulipata athari ya visumbufu vamizi alisema
Bwana luboa.
Hata hivyo Bwana Rubuo
ametoa wito kwa wataalamu walioshiriki katika mkutano huo kuahakikisha wanatoa michango
yao katika kuimarisha mfumo huo ambao utasaidia kuimarisha usalama wa chakula hapa
nchini.
Naye Meneja wa Idara ya
Kilimo Bwana Amithay Kuhanda Amesema wameshirikiana na Wizara ya Kilimo katika kupambana
na kiwavijeshi vyamizi ambao wanachangia kushusha kiwango cha uzalishaji wa mazao
ya wakulima.
Anasema kuwa wanapambana
na kiwavijeshi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki simu janja ambao una saidia kufanya
ufutiliaji wa mashamba yaliovamiwa na kiwavijeshi na kutoa taarifa kupitia mfumo
wa simu hiyo.
Mfumo huu unafanya
kazi zaidi kuanzia ngazi za Kata kufikisha taarifa ngazi ya wilaya kwa haraka
zaidi hiyo kusaidia kutoa taarifa sahihi za maeneo ambayo yameathirika kwa
hatua zaidi.
Mchango washirika hili
la PIC ni kuandaa mfumo ambao unasaidia kuwa tambua viwavijeshi na kufikisha taarifa
haraka kwa wataalamu na watoa maamuzi kwa maaana ya serikali alisema bwana
Amithay Kuhanda.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya uendelezaji wa mazao Bwana ….Malema amelishukuru shirika hilo kwa hatua walizochukua
za kupambana na viwavijeshi vamizi na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha
huduma hiyo inatumika katika mikoa mingi Zaidi.
Bwana malema amesema kwamba
mfumo huo utasaidia kupunguza gharama za ufuatiliaji na ambazo kwa kiasi kikubwa
zilichangia visumbufu hao kuenea kwa kasi
katika maeneo mengine
Hata hivyo alimalizia kwa
kuwataka wataalamu kujifunza tekinolojia hii ili kuwasaidia wakulima na kupunguza
changamoto ya usafriri katika maeneoa mbayo yalikuwa hayafikiki kwa urahisi .
Naye kaimu Mkurugenzi wa
huduma ya Afya ya mimea Bwana Jubilant Mwangi amelishukuru Shirika la PCI
kwa kujana mfumo wa AfriFarma mbao utawasaidia sana wakulima .
Ameshauri mfumo huu
kutumika maeneo mengi Zaidi hapa nchini kwa ajili ya kusaidia kupunguza upotevu
wa chakula ambao unaweza kusababisha hasara kwa wakulima wengi
Aidha amewataka wakulima
wote nchini kutumia mbinu husihi kama IPM mbinu husishi ya visumbufu na kuwa na mitego ambayo
itawakamata kuliko kuongeza matumizi ya madawa yenye kemikali ambayo yanasababisha
kushuka kwa soko la bidhaa husika alisema bwana Jubilant Mwangi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment