Mwezi wa 9 katika kalenda ya kiislamu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni maarufu zaidi kutokana na ibada ya Saumu.
Katika
mwezi huu waislamu hutakiwa kufunga kutoka Machweo mpaka Machwa (Mawio)
katika kipindi ambacho hawatakiwa kula wala kunywa chochote.
Mwezi
wa Ramadhani ni muhimu kwa waumini was dini ya kiislamu kwa kuwa ndio
mwezi ulioteremshwa Kurani na pia hufahamika kama mwezi wa Kurani.
Mbali
na kujiepusha na kunywa na kula Muislamu hutakiwa kujiepusha na maovu
na matendo ya dhambi na kuongeza katika matendo ya ibada kama Swala,
Kusoma Kurani, kutoa sadaka na kadhalika.
Katika nchi nyingi duniani mwezi huu unaanza hivi leo tarehe 27 mwezi Mei mwaka wa 2017.
Ramadan Mubaraq
Mathias Canal
0756413465
Dar es salaam
Mathias Canal
0756413465
Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment