Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William ole Nasha akizungumza katika Kumbukizi ya Miaka 80 ya
Chuo cha Ualimu Butimba iliyofanyika katika chuoni hicho Jijini
Mwanza.
Washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu
waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William ole Nasha wakati wa
kuadhimisha kumbukizi ya miaka 80 ya Chuo cha Ualimu Butimba kilichopo
Wilaya ya Nayamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa wakufunzi wa
Chuo cha Ualimu Butimba ya namna wanavyotumia vifaa vinavyopatikana
katika mazingira wanayoishi kufundishia.
………………………….
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia William Ole Nasha amekitaka Chuo cha Ualimu Butimba kilichopo
Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza kufanya tafakari ya namna gani
kinakuwa chachu ya mabadiliko katika kuandaa walimu wanaoendana na
mahitaji ya sasa.
Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo
Jijini Mwanza wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 80 ya
kuanzishwa Chuo hicho ambapo amesema mijadala itakayoendeshwa ijikite
zaidi katika kujua ni namna gani wanabadili mfumo wa kufundisha ili
wanafunzi waweze kuwa wabunifu na wanaojiamini.
“Nimeona katika maonesho yenu mna jaribu
kufanya masuala ya ubunifu, ubunifu unaanza mwanafunzi akiwa mdogo na
ndio maana tunasema lazima kufanya ufundishaji ambao toka mwanzo unampa
mwanafunzi nafasi ya kuwa mbunifu. Usimbane mwanafunzi jaribu
kumfungulia fursa mbalimbali kwani anapozaliwa anakulia katika mazingira
mbalimbali ya ubunifu hapo utatoa nafasi ya kuweza kuendeleza ubunifu
alio nao,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.
Aliseama Chuo cha Butimba pamoja na
kwamba ni chuo cha ualimu historia yake hasa iko katika ualimu ule wa
Sanaa za maonesho, Sanaa za ufundi ni vizuri kuangalia ni namna gani
Chuo hicho kinarudi katika msatri na kuendelea kutoa walimu ambao
watasaidia katika kufundisha masomo hayo.
“Kwa bahati mbaya kuna mahali tulikosea
kufikiri kwamba music, ufundi, Sanaa za maonesho hazina nafasi katika
elimu, sio vibaya tukarekebisha sababu kama unataka kumfundisha
mwanafunzi ubunifu huwezi kukwepa kutumia Sanaa za maonesho, music na
tamaduni zake zote kwani zinamsaidia kuwa mwanafunzi kamilifu anaeweza
kubuni,” aliongeza Naibua Waziri Ole Nasha
Akizungumzia Jitihada zinazofanywa na
serikali katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia Ole
Nasha amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka historia ya kufanya
uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya elimu kwa kujenga, kukarabati na
kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwenye shule.
Aliongeza kuwa pamoja na mambo mengine
Serikali kuanzia mwaka 2016 inatekeleza Mpango wa Elimu bila malipo,
mpango ambao haujawahi kuwepo ni mara ya kwanza katika historia ya nchi
yetu ambapo inatumia zaidi ya shilingi bil. 20 kila mwezi kugharamia
elimu bila malipo.
Nae Mkuu wa Chuo cha Ualimu Butimba
Huruma Mageni amesema katika kuadhimisha miaka 80 ya Chuo hicho
kinajivunia mambo mengi ikiwemo eneo la chuo kupimwa na kwamba rasimu ya
hati ya chuo iko tayari. Pia inajivunia kuwa na vitengo ambavyo
vinachangia kuboresha elimu katika nchi ya Tanzania
0 comments:
Post a Comment