NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba
amewataka wananchi kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano chini Dakta
John Pombe Magufuli imefanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake na
Ilani yake ya uchaguzi wa Mwaka 2015 tofauti na propaganda za baadhi ya
watu wanavyodai.
Mgumba ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na katika vikao vya wajumbe wa CCM katika Maeneo ya
Kinole.Tegetero na Kibungo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani
Morogoro.
Akizungumza na wajumbe hao kwa nyakati
tofauti Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba ambae ni Mbunge wa Jimbo la
Morogoro kusini Mashariki amesema kuwa serikali imefanya mambo mazuri
katika kuwahudumia wananchi wake katika Jimbo hilo la Morogoro kusini
Mashariki.
Amesema kuwa Baadhi ya miradi hiyo katika
kipindi cha Miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano katika jimbo hilo
ni pamoja kuunganisha mitandao ya Barabara,kutoa fedha kwaajili ya
ujezni ya vituo vya afya,umaliziaji wa maboma na ujenzi wa vyumba vya
madarasa pamoja mabweni ya wanafunzi.
Katika hatua nyingine Naibu waziri wa
Kilimo Omary Mgumba amewataka wananachama wa chama cha Mapinduzi CCM
kueleza mazuri yanayofanywa na serikali kwani wasipofanya hivyo baadhi
ya watu wenye chuki na chama hicho wataeneza propaganda chafu kuwa CCM
haijafanya lolote jambo ambalo halina ukweli.
Pia ametumia fursa hiyo kuwakumbusha
wanachama hao kuchagua viongozi wenye uchungu na CCM pamoja na wenye
kujali maslahi ya wananchi watakao kuja kuwahudumia vizuri.
Kwa uapnde wao Baadhi ya madiwani na
wana-CCM walimpongeza naibu waziri wa Kilimo katika kuwahudumia kwa
kuwaletea maendeleo wananchi wake pamoja na kutatua changamoto
mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili.
0 comments:
Post a Comment