Katibu wa UWT, Wilaya ya Dodoma Mjini,
Diana Madukwa,akizungumza na washiriki wa mafaunzo ya ujasirimali kwa
wanawake ambayo yaliwashirikisha wataalamu kutoka SIDO na Ofisi ya
maendeleo ya jamii.
Afisa Uendelezaji Biashara kutoka
SIDO,akitoa elimu kwa washiriki wa mafaunzo ya ujasirimali kwa wanawake
ambayo yaliwashirikisha wataalamu kutoka SIDO na Ofisi ya maendeleo ya
jamii.
Mratibu Dawati la Uwezeshaji wananchi
kutoka jiji la Dodoma Bi.Hidaya Mizega akitoa elimu na mbinu kwa
washiriki wa mafaunzo ya ujasirimali kwa wanawake ambayo
yaliwashirikisha wataalamu kutoka SIDO na Ofisi ya maendeleo ya jamii.
Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UWT Dodoma
Mjini Mwl.Saphia Mfaki,akizungumza na washiriki wa mafaunzo ya
ujasirimali kwa wanawake ambayo yaliwashirikisha wataalamu kutoka SIDO
na Ofisi ya maendeleo ya jamii.
………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
ZIARA ya Umoja wa Wanawake Wilaya ya
Dodoma Mjini ya kutoa elimu kuhusu ujasiriamali kwa Wanawake
imehitimishwa leo katika Kata za Mihuji, Makole na Uhuru.
Akizungumza katika mafunzo hayo ya
ujasiriamali Katibu wa UWT, Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa
amesema kupitia ziara hiyo ambayo iliwahusisha wataalamu kutoka SIDO na
Ofisi ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake wameweza kunufaika na Elimu hiyo
ya ujasiriamali.
” Tumekua na ziara kwa kata 41 za Jiji la
Dodoma, kote huko tulizunguka na kuzungumzia na akina Mama kuhusu elimu
ya kujitegemea na kujikwamua na umaskini.
” Tunampongeza na Kumshukuru Rais wetu Dk
Magufuli, kwa kuondoa riba katika mikopo inayotolewa na Halmshauri za
Wilaya Nchini kwa wanawake, vijana na walemavu lakini haswa tunamshukuru
kwa kuwakumbuka walemavu ambao ni kundi lililokua limesahaulika katika
suala zima la mikopo.
” Kuna fursa nyingi sana hivi sasa jijini
Dodoma hasa baada ya Rais kuturasimisha kuwa Makao Makuu ya Nchi na
Jiji, ni jukumu letu kama UWT kuandaa mafunzo na warsha mbalimbali za
kuwakomboa Wanawake kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi,” amesema Diana.
Amesema ziara hiyo imekua na mafanikio
makubwa kwani imechangia idadi kubwa ya wanawake kujiunga katika vikundi
vidogo vidogo ambavyo vitawasaidia kupata mikopo Jiji huku wengine
wakienda SIDO kupata mafunzo kamili ya fani mbalimbali.
Kwa upande wake Afisa Uendelezaji
Biashara SIDO, Crispin Kapinga amesema muamko wa Wanawake katika
kujiunga na SIDO ili kupatiwa mafunzo mbalimbali umekuwa ni mkubwa baada
ya ziara hiyo ya UWT.
” Hakika UWT Wilaya ya Dodoma Mjini,
wanastahili pongezi. Wamezunguka Kata zote kutoa elimu kwa akina Mama Na
Vijana ili waweze kujiajiri fursa ni nyingi sana kwenye Jiji letu hivi
sasa.
” Mfano kuna akina Mama ambao baada ya
kupata mafunzo haya wamekuja pale SIDO kwenye ofisi zetu kufundishwa
jinsi ya kutengeneza mifuko mbadala na sasa uchumi wao umekua mkubwa
kutokana na uhitaji wa mifuko hiyo kwa saa, nitoe rai kwa Taasisi
nyingine kuiga mfano huu wa UWT katika kutoa elimu kwa vijana na akina
mama,” amesema Kapinga.
Nae Hidaya Mizega ambaye ni Mratibu
dawati la uwezeshaji Jiji la Dodoma, amewataka wanawake Wilayani humo
kujitokeza kwa wingi katika kuchukua mikopo inayotolewa na Manispaa ya
Jiji la Dodoma kwa Wanawake, Vijana na Walemavu.
“Tunapaswa kuwashukuru UWT Wilaya ya
Dodoma kwa kuandaa mafunzo haya, ni ombi langu kwenu akina Mama
kujihamasisha nyie wenyewe pamoja na watoto wenu kuanzisha vikundi vya
ujasiriamali ili kuweza kupatiwa mikopo.
” Wanawake ndio uti wa mgongo wa Familia,
hampaswi kuwa tegemezi, tuamke tuzikimbilie fursa lakini tusiamke peke
yetu, tuwashike mikono na Vijana wetu waache kukaa vijiweni,” amesema
Hidaya.
Mmoja wa akina Mama waliohudhuria Mafunzo
hayo, Amina Abdallah ameushukuru Uongozi wa UWT Wilaya ya Dodoma kwa
kuandaa mafunzo hayo ambayo yamewafungulia njia katika kujikwamua
kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment