Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama
akihutubia watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano
wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa
Umma inayoendelea ambayo iliambatana na mafunzo kuhusu masuala ya
utumishi wa umma kwa watumishi hao.Mkutano huo ulifanyika Juni 22, 2019
Ukumbi wa mikutano wa PSSSF Jijini Dodoma
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi
akizungumza na watumsihi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa
mkutano huo.Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy
Mwaluko akizungumza na watumsihi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati
wa mkutano huo.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo
pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya
kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma inayoendelea.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akikata keki kuadhimisha siku yake ya
kuzaliwa, keki aliyoandaliwa na watumishi wa ofisi yake kumpongeza
wakati wa mkutano wa kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma
kwa ofisi hiyo.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimlisha keki Mkuu wa Kitengo cha
Mawasilino Serikalini cha ofisi hiyo Bw. Agustino Tendwa kwa niaba ya
watumishi wa ofisi yake, wakati wa mkutano wa kuhitimisha mafunzo ya
masuala ya utumishi wa umma Juni 22, 2019.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi
wa Rasimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Mazoea Mwera akifafanua jambo
wakati mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………..
NA MWANDISHI WETU
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu Waaswa
Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao
ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano
kutoa huduma Bora kwa wananchi.
Akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo
leo (22 Juni, 2019) Jijini Dodoma , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza uwajibikaji,
uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika utumishi wa
umma ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.
“Kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi wa
umma katika Ofisi yetu kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kuwa jambo
hilo halikubaliki kamwe kwani vitendo hivyo vinazorotesha juhudi za
Serikali kuwaletea wananchi maendeleo “ Alisisitiza Mhe. Mhagama
Akifafanua amesema kuwa mafunzo
yaliyotolewa na Serikali kwa watumishi hao ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma yalijikita katika
mada mbalimbali ikiwemo Rushwa mahala pa kazi , haki na wajibu wa
watumishi wa umma.
Aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inaweka
mkazo katika kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vizuri pale
wanapohitaji huduma hivyo ni wajibu wa kila mtumshi katika Ofisi hiyo
kuendelea kutoa huduma bora kwa wale wote wanaofika katika Ofisi hiyo na
katika Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.
Kwa upande wake Katibu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi amesema kuwa watumishi
wa Ofisi hiyo watazingatia maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mhagama
ili kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi.
Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo
wameadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kushiriki mafunzo ya
kuwakumbusha taratibu na kanuni za utumishi wa umma, mafunzo kwa
watumishi wanaotarajia kustaafu hivi karibuni.
Ofisi ya Waziri Mkuu imeadhimisha wiki ya
Utumishi ya Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali na kuhitimisha kwa
mafunzo ya siku moja kwa watumishi wote yakilenga kuwakumbusha wajibu
wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili hatimaye kufikia
malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu inasema; “Uhusiano kati ya
uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi
wa
Masuala ya Uhamiaji; kujenga
utamaduni wa utawala bora., Matumizi ya tehama na ubunifu katika utoaji
wa huduma jumuishi“
0 comments:
Post a Comment