Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na
Watumishi wa ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokutana nao kujadili
utendaji kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu
wa Ofisi hiyo, Bw. Peter Kalonga akieleza jambo kwa watumishi wa Ofisi
hiyo (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maaadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa
Ofisi hiyo wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani)
walipokutana Jijini Dodoma.
Mmoja wa Watumishi wa Ofisi hiyo Bi.
Grace Kigula akielezea baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika
utendaji walipokutana na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakimsikiliza kwa makini
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe alipokutana nao kusikiliza
maoni na changamoto wazokabiliana nazo katika utendaji kazi wao.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) akifafanua
jambo kwa wadau (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo la
kujadiliana pamoja na kusikiliza maoni, ushauri na changamoto
wanazokutana nazo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma mwaka 2019. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura na kulia ni Mwanasheria kutoka
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzan Ndomba.
Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura (kushoto) akifafanua jambo
kuhusu masuala ya vyama vya wafanyakazi wakati wa mkutano huo
uliofanyika ghorofa la PSSSF, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi
ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.
Mwanasheria kutoka Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE), Bi. Suzan Ndomba akielezea kuhusu baadhi ya Sheria
zinazowaongoza Waajiri nchini wakati wa kikao na Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe
(katikati) alipokutana na wadau mbalimbali wa ofisi hiyo. Kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.
Johanes Majura
Baadhi ya wadau wakifuatilia maelezo ya
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) walipokutana kujadili masuala
mbalimbali kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa
Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya
Wafanyakazi.
Mmoja wa wadau kutoka Kampuni ya RECO
Engineering Ltd, Bw. Abubakar Mukadam akichangia mada kuhusu masuala ya
vibali vya kazi walipokutana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) ikiwa
ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Sehemu ya ya wadau wakifuatilia maelezo
ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) walipokutana kujadili masuala
mbalimbali kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa
Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya
Wafanyakazi.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………………..
Na; Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe amewaasa watumishi wa
ofisi hiyo kufanyakazi kwa ushirikiano ili waweze kutumiza malengo
waliyojiwekea.
Hayo ameyasema wakati alipokutana na
watumishi wa ofisi yake Dodoma kwa lengo la kuadhimisha Wiki ya Utumishi
wa Umma inayofanyika kila mwaka kuanzia Juni 16 hadi 23 kwa Nchi
Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuonesha mchango wa
Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa
ujumla ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni;
“Uhusiano kati ya uwekezaji wa vijana na
usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Jenga utamaduni wa Utawala bora,
matumizi ya TEHAMA na Ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi.”
Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa
Umma ambayo ipo kisheria Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Ofisi hiyo ina
majukumu makubwa ya kiutendaji hivyo watumishi wanawajibu wa kufanyakazi
kwa kushirikiana na kujenga umoja.
“Ushirikiano katika kazi ni muhimu na
husaidia kuboresha mifumo ya kiutendaji ikiwemo kuwa na mikakati
endelevu ya ofisi, mawasiliano mazuri, kujenga mahusiano mazuri na wadau
na kutoa huduma bora kwa wananchi,” alisema Massawe.
Sambamba na hilo aliwasihi watumishi wa
ofisi hiyo kufanyakazi kwa bidii, weledi, uzalendo na kuwa wabunifu
katika kutekeleza majukumu yao na utoaji wa huduma kwa wadau na
wananchi.
Pia amewashauri watumishi hao kuepukana
na vitendo vya rushwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na maadili ya
Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia haki
na usawa.
Aidha, Katibu Mkuu alikutana na kufanya
kikao na wadau mbalimbali wa nje na alipokea maoni na mrejesho wa huduma
zinazotolewa na Ofisi ya Waziri kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya
Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na
masuala ya Vyama vya Wafanyakazi.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu Bw. Peter Kalonga aliafiki yaliyosemwa na kuahidi kuahidi kufanyia
kazi maagizo hayo ikiwemo suala la ushirikiano na mawasiliano katika
utendaji kazi baina ya watumishi ili kuimarisha mshikamano baina ya
watumishi.
Kwa upande wake alisema kuwa kikao hiko
kimewezesha watumishi wa ofisi hiyo kubadilishana taarifa zaidi za
kiutendaji na kitasaidia kuimarisha ushirikiano
0 comments:
Post a Comment