Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd,
Bi. Zena Mchujuko ambayo inaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na
Grace Entertainment, akizungumza na waandishi wa habari Julai 04, 2019
Mjini Bariadi.
Washiriki wa Shindano la Miss Simiyu 2019 linalotarajiwa kufanyika kesho Julai 06, 2019 Mjini Bariadi.
Mwalimu wa warembo wanaoshiriki Shindano
la Miss Simiyu 2019, Bi. Doreen Robert Pastory akizungumza na waandishi
wa habari Julai 04, 2019 Mjini Bariadi kuhusu shindano la Miss Simiyu
litakalofanyika kesho Julai 06, 2019 Mjini Bariadi.
…………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Rita Paulsen, Hoyce Temu (Miss Tanzania
1999) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997) wanatarajiwa kuwa majaji wa
Shindano la kumsaka Miss Simiyu 2019, litakalofanyika kesho Julai 06,
2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
.
Hayo yamesemwa Julai 04, 2019 na
Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambalo
linaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, wakati
akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi
Amesema kama waandaaji wameamua kuwaleta
majaji hao ambao ni mahiri na wenye uzoefu katika masuala ya ulimbwende
ili kupata Miss Simiyu ambaye atakuwa na uwezo kuuwakilisha mkoa katika
Shindano la Miss Tanzania.
“Tumeamua kuwaleta majaji hawa kwa sababu
ya uzito wa tukio lenyewe, uzoefu na umahiri wao, lengo letu ni kutoa
Miss Simiyu atakayeweza kutuwakilisha katika Miss Tanzania na tuna
uhakika kila mshiriki atapata haki yake” alisema Mchujuko.
Aidha, Mchujuko amesema Mgeni Rasmi
katika Shindano la Miss Simiyu 2019 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kwa upande wa
Burudani Mwanamuziki wa Kizazi kipya Nasib Abdul alimaarufu Diamond
Platinum atatumbuiza shindano hilo.
Kwa upande wake mwalimu wa washiriki wa
Miss Simiyu 2019 Doreen Robert Pastory alibainisha kuwa majaji hao
wanastahili kuwajaji warembo hao huku akiongeza kuwa suala la urembo
linatakiwa kuchukuliwa kama ajira nyingine badala ya kuchukulia kama
jambo la kihuni ambapo alitoa rai kwa Mikoa mingine kuiga jambo hilo
kwani ni ajira kama zilivyo ajira nyingine.
Naye mmoja wa washiriki Rebeka Manoti
amesema wamefundishwa kwa kuzingatia maadili mema, hivyo wana matarajio
makubwa ya kupata mlimbwende atakayepeperusha vyema tasnia hiyo ya
urembo kimkoa ,kitaifa na kidunia.
Jumla ya warembo 15 watachuana katika
shindano hilo na kiingilio itakuwa Shilingi 10,000 (Regular),Shilingi
50,000(Corparate) na Shilingi 100,000(VIP), na Mshindi wa kwanza atapata
zawadi ya Shilingi Milioni moja na washiriki wengine pia watapatiwa
zawadi.
0 comments:
Post a Comment