Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga
akimkaribisha Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet
mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa ajili ya mazungumzo
na Mwenyeji wake
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa sambamba na Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet wakiongoza kikao kazi kati ya Wataalam wa Wizara ya Kilimo Tanzania na Wataalam wa Wizara ya Kilimo ya Misri katika Ukumbi wa Wizara (Kilimo IV) Jijini Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa sambamba na Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet wakati wa majadiliano na Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania na Wataalam wa Wizara ya Kilimo ya Misri katika Ukumbi wa Wizara (Kilimo IV) Jijini Dodoma
Serikali ya Tanzania na Misri
zinatarajia kusainiana mkataba wa makubaliano wa kuanzisha mashamba makubwa ya
pamoja kwa lengo la kuinua kilimo cha ngano, mpunga na pamba
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga mara baada ya kufanya mazungumzo
na timu ya Wataalamu wa kilimo kutoka Misri wakiongozwa na Waziri wa Kilimo na
Ardhi wan chi hiyo, Dk Ezzidine Abu Stiet.
Mhe.
Hasunga amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kushirikiana katia Sekta
ya Kilimo husan katika mazao ya mpunga, ngano na pamba ambapo tande zote mbili
zitakuwa na mashamba ya pamoja.
“Kama
mnavyojua Misri wamepiga hatua katika kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji na
tekinolojia hivyo tumekubaliana mafaniko hayo yahamie hapa nchini.”
Waziri
Hasunga aliongeza: “Baada ya mazungumzo ya kina na makubaliano katika maeneo ya
ushirikiano, tumepeana miezi miwili ili ifikapo mwezi Mei mwaka huu, tutasaini
mkataba wa makubaliano na kuanza utekelezaji.
Amesema
eneo lingine ambapo wamekubaliana ni kuimarisha Vituo vya Utafiti wa mazao ili
kupata mbegu bora na namna bora ya kuzitumia mbegu hizo na pia kuhamisha ujuzi
na zana kutoka Misri ambao utasidia kuinua kilimo hapa nchini.
Waziri
Hasunga alisema kwa sasa Wataalam wa kilimo wa nchi hizo mbili watatumia muda
huu wa miez miwili kutembelea maeneo mbalimbali ili kubainisha maeneo ambayo
yanafaa kwa kilimo.
“Mfano
tuliwaza kupeleka kilimo cha ngano wilayani Misenyi mkoani Kagera lakini
wamesema eneo hilo ni dogo, hivyo wataalamu wa Misri na wale wa Tanzania
watapita maeneo mbalimbali kuangalia maeneo yanayofaa na baadaye tusainiane
mkataba wa makubaliano,” alisema.
Naye
Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri, Stiet alisema wamekuwa na mazungumzo mazuri
na yenye mafanikio na kukubalianakushirikiana katika mafunzo, utafiti na tekinolojia
katika sekta ya kilimo ili kuboresha mazao ya kimkakati ya pamba, mbunga na
ngano..
“Makubaliano
hayo yanaongeza wigo wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ambayo ni ya muda
mrefu, tumekubaliana kuinua kilimo katika mazao matatu kwa manufaa ya wananchi
wa Tanzania. Baada ya kusainiana mkataba tunategemea utekelezaji wa haraka,”
alimalizia.
0 comments:
Post a Comment