Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Tarehe 17 Juni 2019
akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu amepata fursa ya kumtembelea muwekezaji
mzawa wa kusindika Nafaka Bw Deogratius Kumalija katika Wilaya ya Busega.
Akiwa
kiwandani hapo Mhandisi Mtigumwe alipata maelezo kutoka kwa mmiliki huyo kuwa
ameamua kujikita katika usindikaji wa mazao ya Nafaka kutokana na fursa iliyopo
katika kuongeza thamani ya mazao hayo hususani mahindi na Mpunga.
Bw
Kumalija aliendelea kusema kuwa kiwanda hicho cha Mpunga kina uwezo wa kukoboa
Tani 28 kwa siku na alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kupanga madaraja ambapo
kiwanda cha kusaga Mahindi kipo katika ujenzi na punde kitakapokamilika
kitakuwa na uwezo wa kusaga tani zaidi ya 30 za mahindi kwa siku.
Alisema
kuwa Viwanda Hivyo vitasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo na kuondokana na
nchi kuendelea kuuza mazao ghafi.
Kadhalika,
Mhandisi Mtigumwe alimpongeza muwekezaji huyo kuwa aendelee na uwekezaji huo
pia Serikali imekuwa ikisisitiza kuyaongezea thamani mazao ya Kilimo.
Hivyo
mwekezaji kama Bw Kumalija anatimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozw
ana mHe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwa
na uchumi wa kati kupitia Sera ya Viwanda.
Hata
hivyo kwa kuwa na Viwanda kama hivyo vitaongeza ajira na kuhamasisha wakulima
kulima wakiwa na uhakika wa mazao yao na kuyaongezea thamani.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment