Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb)
Na Mathias Canal, Dodoma
Moja kati ya matatizo yanayowakumba watu wengi kwa kizazi cha
sasa ni tatizo la magonjwa mbalimbali ikiwemo uzito, tatizo hili limekuwa
chanzo cha matatizo mengine makubwa na yenye madhara makubwa kwa afya ambayo
wakati mwingine husababisha kifo.
Magonjwa ya moyo, kisukari, shinikio la damu la kupanda na
kushuka, matatizo ya figo na viungo vingine vya mwili pamoja na kukosa mvuto wa
kawaida yanasabishwa na mtu kuwa na uzito ambao anashindwa kuumudu.
Njia pekee ya kukabiliana na kadhia ya magonjwa mbalimbali
mwilini hususani kwa wanaume ni kula vyakula vyenye viungo mbalimbali (Spices)
kwani zina faida nyingi kwenye afya ya wanaume.
Ushauri huo umetolewa tarehe 6 Februari 2019 na Naibu Waziri
wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa wakati wa kipindi cha maswali na majibu
Bungeni Jijini Dodoma.
Madhara ya kutokula vyakula vyenye viungo kwa wanaume
husababisha uzito kuongezeka kutokana na mtindo fulani wa maisha ya mwanadamu
na pia unaweza kupungua kutokana na mtindo huu huu wa maisha ambao kama ukimudu
kuuzingatia hasa kwenye chakula unaweza kupungua uzito na kuishi maisha salama.
Mhe Bashungwa alisisitiza kuwa kumekuwa na malalamiko mbalimbali
kutoka kwa wanaume kuugua magonjwa mbalimbali huku akibainisha kuwa tatizo
linalopelekea kadhia hiyo ni kutokula vyakula vyenye viungo mbalimbali.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment