Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili ya Bima kwa majanga ya kilimo inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya washiriki wa Bima kwa majanga ya kilimo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akifatilia kwa makini mkutano wa Bima kwa majanga ya kilimo mara baada ya ufunguzi inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) na baadhi ya washiriki wa semina ya Bima kwa majanga ya kilimo inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara
ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe
7 Februari 2019 amefungua semina ya siku mbili ya Bima kwa majanga ya kilimo nayofanyika
kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam
Akizungumza katika semina hiyo Mhe Hasunga amesema kuwa hiyo
ni hatua nzuri katika kuhuisha utoaji wa huduma bora za bima za kilimo kwa
kuzingatia matakwa ya Sheria ya Bima ya Mwaka 2009, Sheria na Mipango
Mbalimbali katika sekta ya kilimo; kwa kutafutia ufumbuzi wa pamoja changamoto zinazokabili
sekta ya kilimo na wakulima nchini.
Waziri Hasunga ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi
wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) kwa kuandaa mkutano huo muhimu wa wadau wa
bima katika kilimo kwani utakuwa na fursa ya kujadili na kuchambua namna ya
kuboresha tija kwa wakulima kwa kuwaingiza katika Bima ya Mazao.
Alisema kuwa
jitihada hizo za sekta ya bima nchini ni kuunga mkono mipango ya Serikali ya
Awamu ya Tano
inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwani Viwanda ni
Kilimo, na kilimo bora chenye tija hukingwa na bima.
Amesema
kuwa semina hiyo ikiongozwa na dhima inayosema “Bima za Kilimo Nchini Tanzania: Nafasi na Wajibu katika Utekelezaji” inalenga
kuleta majibu katika changamoto ambazo serikali imejikita katika kukabiliana
nazo hususani kwa wakulima kote nchini.
Aliwataka
Wataalamu wa Bima waliohudhuria katika semina hiyo kutambua kuwa sekta ya bima
ni kichocheo muhimu katika uchumi wa viwanda na Kilimo chenye tija. Kwa kukinga
majanga mbalimbali katika Mnyororo mzima wa sekta ya kilimo kwa sehemu kubwa
kuimarisha viwanda.
Waziri
hasunga amewataka wataalamu katika sekta ya bima na wa upande wa Sekta ya Kilimo
kujiuliza na kujibu maswali ya Kwanini mwamko wa wananchi katika bima hususani
Bima za kilimo upo chini? (kwa mujibu wa takwimu ni 15% tu ya watanzania hupata
huduma za bima) kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na zaidi ya 75% ya
wanojihusisha na kilimo.
Ni
lini na kwa namna gani wakulima na wafugaji wadogo wa Tanzania wataanza
kunufaika na bima za Mazao na Mifugo?, na Njia zipi zitumike kuhakikisha kuwa
huduma za bima za kilimo zinakuwa nafuu na zenye tija katika Sekta za Kilimo, Mifugo
na Uvuvi.
Mengine,
Ni njia zipi zinaweza kutumika kuwahamasisha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutumia
huduma za bima katika kazi zao na Ni jinsi gani Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano inaweza kutumika katika kurahisisha upatikanaji wa huduma za bima
za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Pia,
amehimiza kuelekea lengo la kuhakikisha angalau asilimia 50 ya watu wazima
wanapata huduma ya bima ya chini ifikapo mwaka 2028, kutafakari jinsi Tanzania inavyoweza
kuimarisha teknolojia zinazojitokeza kama vile majukwaa ya biashara ya digitali
na mifumo ya malipo ya simu kutoa huduma za bima na huduma kwa wakulima
wanaofikia milioni 38. Ubunifu na ushirikiano katika kupata masoko mapya hususani
ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kutumia njia mbadala vitaimarisha ubia kati ya
sekta ya kilimo na bima.
Awali,
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt Baghayo Saqware alisema kuwa wazo kuu la kuandaa
mkutano huo ni kuendeleza kwa dhati ushirikiano kati ya Taasisi za Umma,
Makampuni Binafsi na Mashirika ya Kijamii ili kutoa huduma ya Bima ya kilimo
katika jamii kwa wigo mpana.
Alisema
kuwa kuanzia mwaka 2016/2017 serikali ilizindua mpango wa miaka mitano
uliojikita katika kuifanya Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati kwa kutegemea
viwanda.
Aliongeza
kuwa maeneo muhimu ambayo sekta ya Bima (Binafsi) na Taasisi za umma zinaweza
kufanya kazi kwa pamoja ili kuongeza ufanisi katika shughuli za Bima ya kilimo
kwa kuwa na sera ya Taifa ya Bima, Kuwa na taarifa za wakulima (Data Base),
vilevile wananchi kuwa na imani (Kuamini) biashara na huduma za Bima.
Zingine
ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma na wigo wa huduma za Bima nchini,
Teknolojia rahisi na rafiki kwa ajili ya kusambaza Bima, kuuza Bima, Kulipa
mafao/Madai ya Bima, kusikiliza maoni na mahitaji ya wananchi, na kuchakata
maombi ya Bima.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment