METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 14, 2015

MAPINDUZI ISMANI PITIA WASIFU WA MTANGAZANIA HUYU.

HOTUBA YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ISIMANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MWAKA 2015



UTANGULIZI
UTAMBULISHO
Jina langu naitwa FESTO FUNGAMEZA KISWAGA. Nilizaliwa mwaka 1974 katika kijiji cha malinzanga, kata ya Mlowa ,Tarafa ya idodi ,Wilaya ya Iringa vijijini, Mkoa wa Iringa. Mimi ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano katika familia ya Mzee Fungameza Kiswaga. Mzee Kiswaga alikuwa Mkulima wa Kawaida katika Kijiji cha Malinzanga ,kata ya Mlowa ,wilaya ya Iringa Vijijini.
TAALUMA
·       Shahada (Degree) ya sayansi ya usimamizi wa wanyamapori kutoka chuo Kikuu cha Dar-es-salaam (2007-2010)
·       Diploma ya usimamizi wa Maliasili Chuo kikuu cha maliasili, Mweka, Moshi (2001-2003)
·       Elimu ya sekondari Mkwawa high school (1993-1995)
·       Elimu ya Sekondari (1989-1992) Malangali sec school
·       Elimu ya Msingi (1982-1988) shule ya msingi Mlowa Iringa vijijini.
MAFUNZO MBALIMBALI
·       Kozi ya usimamizi wa shughuli za maendeleo kwa nchi zinazoendelea ; Nanchang, Shanghai na Beijing –China (2014)
·       Kozi ya namna ya tathimini maendeleo ya watu katika nchi za afrika Tripoli,Libya (2010)
·       Kozi ya masuala ya usimamizi rasilimali na usalama maeneo ya mipakani, Nairobi-KENYA (2007)
·       Kozi ya mafunzo ya uendeshaji wa bima ya afya ,Mtwara (june,2014)
·       Kozi usimamizi wa mipaka ya nchi na ulinzi wake, Nairobi (july,2006)
·       Kozi ya ufuatiliaji ya uboreshaji wa shughuli za kilimo , Manyara (May, 2005)
·       Mafunzo ya juu ya uongozi na kuzuia ugaidi Kutoka Max International Security academy, Tel viv, Israel (2007)
·       Mafunzo ya kozi ya kutunga sera na kuondoa umasikini  Arusha,2014
·       Kozi ya uendeshaji mashirika makubwa (Novotel hotel, 2004)
·       Kozi ya uongozi na itikadi ya chama, 2009 (Makao makuu ya Chama -Dodoma)
·       Kozi ya viongozi wakuu wa serikali za Wanafunzi wa vyuo vikuu wa afrika mashariki, 2010 Kigali-Rwanda.
·       Kozi mbalimbali za usimamizi wa rasilimali na ulinzi wa watu.
 
UZOEFU WA UONGOZI
Ndugu zangu wana isimani mimi nina uzoefu wa wa uongozi kama ifuatavyo;-
·       May 2015 mpaka ninavyoongea sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi,Bukoba –mkoa wa Kagera
·       Feb –May 2015 Mkuu wa wilaya Mvomero, Morogoro
·       May 2012-Feb 2015 Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu,Mkoa wa Mtwara.
·       2005-2012- Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Usalama Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) –Hifadhi ya Serengeti,Mkoani Mara.
·       2007-2008- Nilichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam. Baada ya kufanya vizuri katika kuwawakilisha wanafunzi wenzangu mwaka 2009-2010 nilichaguliwa kuwa Rais wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar-es-salaam (DARUSO)
·       2009-2010-Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Katika Chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM)
·       2009-2011-Nilichaguliwa kuwa Rais wa umoja wa shirikisho la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki ambapo inashirikisha zaidi ya vyuo 400 vya elimu ya juu katika nchi za Tanania,Kenya,Uganda, Rwanda na Burundi. Ushindi huu wa kuwa niliupata katika mkutano uliofanyika July 2009 mjini Nairobi, nchini Kenya- Ulikuwa ni ushindi wa heshima kwa nchi yetu Tanzania kwani wagombea walikuwa watano kutoka nchi zote na mimi nilichaguliwa kwa kishindo ambapo nilipata asilimia 76 ya kura zote.
·       2001-2003-Makamu wa Rais wa serikali ya Wanataaluma wa chuo kikuu cha Kimataifa cha Wanyamapori,Mweka –Moshi,Kilimanjaro. Wakati huo huo 2001-2003-Mjumbe wa Bodi Chuo kikuu cha Wanyamapori-Mweka,Moshi –Kilimanjaro.
·       2003-2005-Mkuu wa kanda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mkoa wa Iringa.
·       1996-2001- Mwenyekiti wa Mradi wa MBOMIPA, mradi ambao unashirikisha vijiji 21 katika Tarafa za Idodi na Pawaga- Nafasi ilionisaidia kufahamu vizuri tarafa za Pawaga na Idodi hasa katika eneo la changamoto na fursa za vijiji vyote 21 vya eneo hili la mradi.
·       Nilishawahi kushika nafasi nyingine mbalimbali katika kampuni za uwindaji wa kitalii na taasisi zingine.
·       2012- 2015-Katibu wa Wakuu wa Wilaya ya Mtwara, pia Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya ya Morogoro Feb 2015.
·       Kozi ya maendeleo ya binadamu katika ulimwengu wa Anuwai, UNDP, 2009 Nairobi, Kenya.
 
TUNZO NILIZOWAHI KUTUNUKIWA
·       Tunzo ya uongozi uliotukuka kutoka chuo Kikuu cha Dar-es-salaam
·       Tunzo ya uongozi uliotukuka kutoka chuo kikuu cha wanyamapori ,Mweka Moshi.
·       Tunzo ya uongozi kutoka taasisi inaojishughulisha na Elimu katika vyuo vikuu vya Africa mashariki.
·       Hati iliotukuka kutoka chuo cha mafunzo ya ulinzi wa raia- Insitute of terrorism research and response, Israel.
·       Cheti cha usimamizi uliotukuka katika mkutano wa dunia wa kujadili maendeleo duniani; kutoka taasisi ya World Economic Forum, uliofanyika-Dar-es-salaam, Tanzania 2010.
UONGOZI KATIKA CHAMA
·       2012 mpaka sasa ;Mjumbe wa kamati ya siasa CCM wilaya        (kwa cheo changu)
·       2012 mpaka sasa; Mjumbe wa halmashauri kuu mkoa kupitia kata ya Mlowa
·       2007-2012 Mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Iringa vijijini (wajumbe 10 wa kuchaguliwa na mkutano mkuu).
·       Mwenyekiti wa kamati ya vijana wa CCM katika mkutano wa semina ya viongozi vijana wa CCM 2010; Dodoma.
 
HISTORIA YA JIMBO LA ISIMANI
Jimbo la Isimani lipo katika Wilaya ya Iringa, Jimbo hili lina tarafa 3 yaani Isimani, Pawaga na Idodi. Jimbo hili lina Kata kumi na tatu; ambazo ni Kising’a, Kihorogota, Malengamakali, Nyang’oro,Izazi na Migoli. Zingine ni Mboliboli (kata Mpya), Itunundu, Mlenge,ilolompya, Mlowa,idodi na Mahuninga.
Jimbo hili linabeba jina maarufu katika maendeleo ya Tanzania kwani isimani katika miaka ya sitini mpaka themanini mwanzoni isimani ilisifika kwa kilimo cha zao maarufu ya chakula zao la mahindi. Hii ndio ilipelekea Hayati Mwalimu Nyerere kujenga Ghala la Taifa la Chakula Mkaoni Iringa ghala ambalo lipo mpaka leo japo harihifadhi mahindi ya kutoka isimani tena kwa sababu ya kuporomoka kwa kilimo hiki kwa sababu mbalimbali. Kwa ujumla wake jimbo la ismani kwa maana isimani yenyewe,pawaga na Idodi tarafa zote zimejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo hazijaendelezwa na kuwekewa mikakati ambayo itasaidia kuinua hali ya maisha ya sisi wananchi tunaoishi katika jimbo. Hata hivyo Jimbo hili ambalo linabebwa zaidi na maendeleo ambao ni ya kitaifa na hivyo kuwa ni moja ya jimbo yanayotegemea mipango ya mpito (yaani maendeleo ambao ni mipango unganishi ya Mikoa na Wilaya zingine); Mfano Jimbo hili lipo katika njia kuu ya Mbeya kwenda Arusha kupitia Dodoma hivyo kujikuta barabara kuu hii ambao katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais wa Jamhuri Muungano Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameijenga kwa Kiwango cha Lami (barabara hii inatoka iringa Mjini kupitia eneo la jimbo la isimani,eneo la jimbo la mtera,Dodoma mpaka Arusha. Bahati nyingine ni kwamba barabara nyingine inatoka iringa Mjini kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Kwa upande wa miundombinu ya barabara a halmashauri mkurugenzi wa Halmashauri amekuwa anajitahidi sana kuhakikisha barabara hizi zinapitika muda wote katika kipindi chote cha mwaka. Hata hivyo ipo changamoto kubwa kwa baadhi ya vijiji kutounganishwa na mtandao wa barabara katika eneo kubwa la jimbo.
HALI YA SASA KIUCHUMI NA MAENDELEO YA WATU
Ukiachilia mbali suala la barabara jimbo la isimani kwa ujumla liko katika hali mbaya kiuchumi; Tarafa ya Isimani ambao jamii katika kata za kising’a, kihorogota, malengamakali, na nyangoro asilimia 100 zinategemea kilimo na ufugaji; ilitegemea kilimo imekuwa inaporomoka kiuchumi mwaka hadi mwaka, hali ni si nzuri na ikiachwa namna ni hatari na haivumiliki. Kwa sababu in madhara makubwa sana katika maendeleo ya jamii husika. Pamoja na tatizo la mvua kuwa chache lakini umekosekana ushirikishwaji wa jamii husika yaani pengo kubwa na wananchi hawa pamoja na ari kuwa walionao ya kujiletea maendeleo kimekosekana kiungo muhimu sana kati ya wananchi na taasisi za utafiti wa kilimo ambapo katika maeneo mengine amabao yapo na hali ya kama ya isimani uzalishaji wa mazao umekuwa unapanda mwaka hadi mwaka. Kwa nini isimani tu? . Jamii za kata za Izazi na Migoli na wakulima,wafugaji na uvuvi jamii ya eneo hili nazo kiuchumi inazidi kushuka tena kwa kiwango cha kutisha,  jamii za maeneo haya uchumi wao unashuka kwa sababu ya kukosa msaada ya ushauri mbinu za kilimo, uvuvi na ufugaji, katika eneo hili katika kipindi cha miaka thelathini wananchi hawajawahi kupata msukumo wa ni namna gani wanaweza kurudi katika uchumi waliowahi kumiliki miaka ya nyuma wamebaki bila matuamini yoyote
 
Ni lazima hali hii inatafutiwa mikakati ya kukabili haraka sana kwani tayari imeshaleta athari kubwa kiuchumi na kijamii katika tarafa hii iliosheheni udongo wenye rutuba sana na yenye jina kubwa.
 
Tarafa ya pawaga ambao kwa uhakika ina hazina ya ardhi yenye rutuba na miundombinu ya umwagiliaji, asilimia kubwa ya jamii inajitegemea katika kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyakazi. Utegemezi huu unarudisha nyuma jitihada na uchapakazi wa jamii hii. Pamoja na tarafa hii kuwa na bahati ya kuwa katika eneo hili bado kipato katika kilimo cha mpunga hakina record nzuri ya kupanda kwa sababu ya kukosa mikopo kwa wakulima wadogo ili kuwawezesha kuingia katika ukulima wakati na mkubwa kama ilivyo katika mabonde mengine ya Dakawa-morogoro, kilombero na mbarari. Hii imedumaza sana uchumi wa wananchi wa Pawaga.  Jitihada kubwa inaotumika na wakulima hao inahitaji msaada wa kuwasukuma ili waweze kwenda mbele kwa kasi zaidi kwa vile kila kitu wanacho hili lazima lishughulikiwe sasa na sio baadae. Wafugaji wa eneo lote la jimbo la ismani hawajawahi kushirikishwa katika kuwatambua na kuwapa misukumo ili nao wachangie pato la jimbo kwa sababu wameachwa kila mfugaji anahaingaika na mifugo yake hii haikubariki hata kidogo.
Eneo la kubwa la tarafa inapakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha na pia pori tengefu la Lunda Mkwambi. Pamoja na hali hii wananchi wamekuwa hawafaidi chochote kutoka katika eneo hili bali wamekuwa wanapata adha kubwa na wanyamapori waharibifu kama tembo na wanyama wengine. Kibaya zaidi kuna mradi wa MBOMIPA ambao ndio lnapaswa kuwa mukombozi wa vijiji hivi lakini matokeo yake mradi huu umekuwa unamilikiwa na watu wachache na wananchi hawashirikishwi tena kama inavyopaswa kuwa. Ikumbukwe wakati mradi huu unaanzishwa wananchi walishirikiswa lakini sasa umekuwa wa wachache na wananchi wamekosa imani na wasimamizi wa mradi huu maana sio wao tena.
 
Tarafa ya Idodi, ni tarafa ambayo ina rutuba ya kutosha kwa kilimo na ndio tegemeo kubwa la jamii ya eneo hili. Kama ilivyo isimani jamii na wananchi tumekosa matumaini ya kilimo kwa sababu ya kukata tamaa. Miundombinu ya umwagiliaji hakuna wakati upo uwezekano wa kuweka upo. Katika kata ya mlowa ahadi za kujengewa kwa muundombinu huu imekuwa ya muda mrefu na mpaka sasa haijakamilika.
Eneo la Idodi kuna changamoto za migogoro ya wakulima na wafugaji, wanyama waharibifu na uchumi uliodumaa. Kumekosekana na ushauri wa kuondokana na hali ya umasikini ambao unaendelea kushamiri katika tarafa hii. Kazi nzito inafanywa na wananchi katika kujiletea maendeleo inaishia katika kuhangaika na kilimo kisicho na kipato cha maana. Kwa tafsiri ni lazima mfumo na namna ya kushughulikia uchumi wa tarafa hii uanze mara moja bila kuchelewa.
 
CHANGAMOTO ZILIZOPO
Ni jukumu la kiongozi yeyote makini anapotaka kugombea uongozi katika ngazi mbalimbali kujua changamoto na kuibua fursa zinazopatikana katika ndani na nje ya eneo husika ili kuhakikisha wananchi wanapata unafuu wa maisha na pia kujielewa muskabali wao na watoto wetu. Hata hivyo changamoto nyingi sana katika jimbo hili zimekosa kiongozi mwenye uchungu kami mimi.
Katika tafakari hiyo jimbo la isimani linakabiliwa na tatizo la maji. Ikumbukwe kuwa jimbo hili linapitiwa na mto Ruaha mdogo katikati, mto huu hutiririsha maji mwaka mzima. Pia jimbo hili kwa upande wa magharibi kuna bwawa kubwa la mtera ambalo pia hukaa mwaka mzima wa mwaka. Lakini jimbo hili asilimia 70 lipo uwanda wa chini ambao ni rahisi kushughulikia maji kwa gharama nafuu kwa maji kusambazwa kwa mtiririko (gravity) pamoja na kuwa na bahati hiyo kuna tatizo kubwa sana la maji.
Kwa ujumla tangu jimbo hili lizaliwe miaka zaidi ya ishirini iliyopita tatizo la maji halijashughulikiwa kwa kiwango cha kuridhisha. Nikipata ridhaa ya CCM na Hatimaye kuteuliwa kuwa Mbunge nitahakikisha njaa inabakia historia ili wananchi waungane na wenzao majimbo mengine wanaofurahi hali bora ya huduma za jamii na hasa maji.
HALI YA MAJI JIMBONI
Serikali yetu imetekeleza miradi mbalimbali katika azima ya kusogeza huduma za maji jirani na wananchi. Miradi ya maji kupitia benki ya dunia, na pia za Sweden.
Kuna jitihada zimefanyika kupitia wadau wa maendeleo yaani Familia ya Huwel hususani mr sarehe na Ahmed. Kuna kazi nzuri imefanywa na kanisa Katoliki na pia kanisa la anglikana; wadau hawa wa maendeleo ninawapongeza sana kwa kazi nzuri.
Hata hivyo jimbo hili bado lina shida kubwa sana la maji ya kunywa na kwa ajili ya mifugo na matumizi mengine. Ahadi nyingi za wananchi kutupatia maji nyingi zimedumu miaka mingi na hazina dalili za kukamilishwa. Kwa hiyo zinahitaji msukumo mpya na mtu pekee anayeweza kukabiliana matatizo haya ni mimi.
Sisi wananchi wa Isimani kwa umoja wetu tunaweza, tunaweza. Mipango ya namna ya kukabilna na suala hili nitaliekeza wakati wa kampeni zangu kuanzia tarehe 20 july 2015.
KILIMO
Kama nilivyoeleza hapo juu sekta ya kilimo katika jimbo la isimani imekufa, sekta hii imekufa kwa sababu ya kukosekana kwa mbinu mbadala za kuendeleza kilimo. Matokeo yake tunaaminishwa kuwa tutaletewa chakula cha msaada; sisi wananchi wa isimani tutajipanga kurudisha heshima yetu kwa kurudisha kilimo cha kisasa na mbegu za kisasa zitatafutwa kokote ziliko ili ziwe isimani. Kazi hii haijafika toka miaka thelathini iliyopita . mipango yangu nitaiweka hadharani wakati wa kampeni.
Njaa katika jimbo hili inataka kuzoeleka kama vile ni jambo zuri. Nikipata ridhaa ya CCM na Hatimaye kuteuliwa kuwa Mbunge nitahakikisha njaa inabakia historia ili wananchi waungane na wenzao majimbo mengine wanaofurahi hali bora ya chakula.
BARABARA
·       Halmashauri ya wilaya ya iringa imejitahidi kufanya matengenezo kwa barabara lakini zipo barabara muhimu ambazo hazijafunguliwa ili kufufua uchumi na mawasilaiano miongoni mwa wana ismani.
AFYA
·       Huduma za afya bado katika vijiji na maeneo bado haziridhishi, mipango yangu katika eneo hili nitazileza katika kampeni zangu.
ELIMU
·       Kuna vijana wengi wamemaliza form four na vyuo vikuu wapo vijijini. Nitaeleza mipango wakati wa kampeni zangu.
UMEME
·       Naomba nimshukuru DR Jakaya Mrisho Kikwete kwa kazi nzuri ya kupeleka umeme vijijini ambapo vijiji zaidi ya 3000 nchi nzima ambapo kupitia REA viijiji vinawaka. Hata hivyo kumekuwepo na upendeleo kwa baadhi ya vijiji hawajapata na vitongoji katika vijiji vingi bado haujapelekwa. Majibu ya suala hili yamekuwa ya kukatisha tama
HITIMISHO
Jimbo hili lina fursa nyingi ambazo kwa makusudi au kwa bahati mbaya hazijatumika kwa malengo maalumu. Ninaomba leo niwajulishe wanaisimani kuwa muda utakapofika nitachukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la isimani. Fursa hii ni muhimu sana kwa wanaisimani wenzangu ambao wamevumilia kwa kipindi kirefu shida wanazokabilina nazo ambazo sasa zitapata uvumbuzi kupitia kwangu endapo wanaismani mtanipa ridhaa ya kuwatumikia.
Festo kiswaga
Mtangaza nia pia ni Dc msenyi-mkoani Kagera.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com