METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 1, 2019

RAIS MSTAAFU MWINYI AKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI KURANI KIKWAJUNI

Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Kumi na Tano, Abdallah Hassan, akibeba zawadi ya televisheni aliyokabidhiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (watatu kushoto), wakati wa fainali za mashindano yaliyofanyika leo  katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.

Rais  Mstaafu  wa  Awamu  ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi zawadi  Mshindi  wa  Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Tano, Asia Abdallah  wakati  wa fainali za mashindano hayo yaliyofanyika leo, katika Viwanja  vya  Mapinduzi, Visiwani  Zanzibar.Wakwanza  ni  Mbunge  wa  Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi  Hamad Masauni.

Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani katika Jimbo la Kikwajuni, Thureiya  Abdallah  akisoma  Kurani  wakati  wa  mashindano  hayo  yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Mbunge  wa  Jimbo  la  Kikwajuni, Mhandisi  Hamad  Masauni (kulia), akimkabidhi  zawadi  Mgeni Rasmi  katika  Mashindano  ya  Kuhifadhi  Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji  Ali  Hassan  Mwinyi.Mashindano hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa  Mjiini, Twalib Ali Twalib  akikabidhi  msaada  wa  vitabu  vitakavyoenda katika madrasa mbalimbali Visiwani  Zanzibar  kwa  Mgeni  Rasmi  katika  Mashindano  ya  Kuhifadhi Kurani, Rais  Mstaafu  wa  Awamu  ya  Pili, Alhaji  Ali  Hassan Mwinyi, wakati wa Mashindano  ya  Kuhifadhi  Kurani  yaliyofanyika  leo Visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na anayefuatia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Salehe Nassor JazzeraPicha na Mpigapicha Wetu

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com