METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 1, 2019

SERIKALI YAJIPANGA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO YA MALISHO YA MIFUGO NCHINI

Na. Edward Kondela

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wizara hiyo ina mpango wa kuondokana na changamoto ya malisho ya mifugo ambayo imekuwa ikisababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Prof. Gabriel amesema hayo katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, kwenye hafla fupi ya kupokea matrekta saba kwa ajili ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) pamoja na Shamba la Malisho Vikuge kupitia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO unaofadhiliwa na Serikali ya Poland.

Akizungumza katika hafla hiyo katibu mkuu huyo amesema matrekta manne ambayo yamenunuliwa na TALIRI kwa njia ya mkopo wa miaka miwili wenye thamani ya takriban Tshs. Mil 220 na matrekta matatu ambayo yamenunuliwa kwa fedha taslimu Tshs. Mil 192.1 na Ofisi ya Msajili Hazina kwa ajili ya Shamba la Malisho Vikuge, yatatumika kwa ajili ya kilimo kwenye mashamba ya malisho ya mifugo na kuongeza wingi wa upatikanaji wa malisho na yenye ubora kwa mifugo pamoja na kuondoa migogoro ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika mashamba ya wakulima pamoja na ufugaji wa kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho.

“Wizarani tunataka kuondokana na tatizo la malisho katika nchi hii ambalo limeainishwa kwenye ibara ya 25 katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, changamoto ya malisho ni kubwa kwa wafugaji tunaamini tutakapoondokana na changamoto ya malisho, changamoto ya maji tutapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyopo, tutapunguza tatizo la ubora wa mifugo yetu, ndiyo maana tumeamua kuanzia Shamba la Malisho Vikuge.” Alisema Prof. Gabriel

Katibu mkuu huyo pia ameitaka TALIRI kuhakikisha matrekta hayo yanatumika ipasavyo kwa ajili ya kuzalisha kwa kutumia mtaji huo na kulipa deni kwa wakati ili taasisi nyingine za serikali zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ziweze kunufaika na mkopo huo ikiwemo Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) ambayo imekuwa na mashamba makubwa ya uzalishaji wa mifugo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof. Damian Gabagambi, shirika ambalo linasimamia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO amesema faida ambayo wanataka kuiona kupitia mradi huo hapa nchini ni kubadilika kutoka kilimo cha mkono hadi kilimo cha kutumia matrekta.

“Serikali ilipoanzisha mpango huu haikuanzisha ili kupata faida kama wafanyabiashara wengine, faida ambayo serikali inatarajia kupitia mpango huu ni kilimo kilichobadilika, kilimo ambacho kinaondoa jembe la mkono kwa hiyo kupitia mradi huu, serikali imejipanga kupeleka jembe la mkono makumbusho.” Alisema Prof. Gabagambi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI Dkt. Eligy Shirima na Meneja wa Shamba la Malisho Vikuge Bw. Richard Mdegipala wamesema wanatakiwa kuleta mabadiliko katika sekta ya mifugo hususan kwa kuboresha malisho ya mifugo na kuondokana na tabia ambayo wafugaji wengi wanatumia kwa miaka mingi ya kutafuta malisho ya mifugo yao porini.

Aidha wamesema matrekta hayo yatatumika pia na majirani wa taasisi ya TALIRI pamoja na Shamba la Malisho Vikuge na kwamba matrekta hayo yatawawezesha kuongeza gawio kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Hadi sasa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kupitia mradi wa kuunganisha matrekta wa URSUS-TAMCO limeshauza matrekta 413 katika maen

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com