METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 1, 2019

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AONGOZA OPARESHENI YA UKAGUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI JIJINI DODOMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo akiongea wakati wa uzinduzi  wa operesheni ya zuio la mifuko la mifuko ya plastiki ilyofanyika jijini Dodoma ikiwa ni agizo la Serikali kuwa ifikapo tarehe 1 juni hakuna tena kutumia mifuko ya plastiki

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha kuzuia mifuko ya plastiki jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa operesheni ya kukagua mifuko ya plastiki jijini humo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Joseph Malongo akiwa pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Dodoma wakati wa ukaguzi wa mifuko ya plastiki kwenye maduka na masoko jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo akinunua kikapu ikiwa ni kuhamasisha viongozi kutumia mifuko mbadala  na kuachana na mifuko ya plastiki jijini Dodoma

Sehemu ya Wakazi wa jiji la Dodoma waliohudhuria katika uzinduzi wa operesheni ya ukaguzi wa mifukoya plastiki jijini Dodoma.

…………………..

Wito umetolewa kwa Wakazi wa Dodoma na Wilaya zake  kuacha kabisa kautumia mifuko ya plastiki na kuanza mara moja matumizi ya mifuko mbadala ikiwa ni kutii agizo la Serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo wakati wa uzinduzi wa operesheni ya kukagua mifuko ya plastiki katika jiji la Dodoma ambapo ni kutii agizo la Serikali la ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia juni 1.

Akiongea katika oparesheni hiyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo Wasimamizi wakubwa wa mazingira Nchini, hivyo amefurahi kuona elimu juu ya katazo la mifuko ya plastiki kwa jiji la Dodoma imefika kwa Wananchi kwa sababu ambao wamekutwa na mifuko ya plastiki ni wachache sana kulinganisha na Wananchi wanaotumia mifuko mbadala kwa siku ya leo. ‘Elimu imefika kwani kila Mwananchi namuona kabeba mfuko mbadala, vikapu n.k” alisema Injinia Malongo

Naye Mkuu wa Wilaya wa jiji la Dodoma Mh. Protabas Katambi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na anawaagiza Wananchi na Wafanyabiashra wa jiji laDodoma  kutii agizo la Serikali na kuachana kabisaa na matumizi ya mifuko ya plastiki. ‘Mwananchi atakayekutwa na mfuko wa plastiki hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake, hili suala syo mchezo mchezo nia agizo la Serikali” alisema Katambi

Operesheni hiyo ya kukagua mifuko ya plastiki imekuja baada ya Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kutoa agizo bungeni kuwa ifikapo juni 1 hakuna Mwananachi atakayeruhusiwa kutumia mifuko ya plastiki Nchini Tanzania.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com