RAIS MSTAAFU MWINYI AKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI KURANI KIKWAJUNI
Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani
Juzuu Kumi na Tano, Abdallah Hassan, akibeba zawadi ya televisheni
aliyokabidhiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan
Mwinyi (watatu kushoto), wakati wa fainali za mashindano yaliyofanyika
leo katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji
Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Mashindano ya
Kuhifadhi Kurani Juzuu Tano, Asia Abdallah wakati wa fainali za
mashindano hayo yaliyofanyika leo, katika Viwanja vya Mapinduzi,
Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,
Mhandisi Hamad Masauni.
Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi
Kurani katika Jimbo la Kikwajuni, Thureiya Abdallah akisoma Kurani
wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika leo katika Viwanja vya
Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,
Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi
katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya
Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.Mashindano hayo yamefanyika leo katika
Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Mkoa wa Mjiini, Twalib Ali Twalib akikabidhi msaada wa vitabu
vitakavyoenda katika madrasa mbalimbali Visiwani Zanzibar kwa Mgeni
Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Mashindano ya
Kuhifadhi Kurani yaliyofanyika leo Visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia
ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na anayefuatia
ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Salehe Nassor JazzeraPicha na Mpigapicha Wetu
No comments:
Post a Comment