METDO Tanzania

METDO Tanzania
Showing posts with label Habari za Jamii. Show all posts
Showing posts with label Habari za Jamii. Show all posts

Friday, March 18, 2022

KATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUKA UKAMILISHAJI WA AWAMU YA KWANZA YA UUNDWAJI WA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA HUDUMA ZA PAMOJA KWA WAWEKEZAJI





KATIBU Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara Prof. Godius Kahyarara ameitembelea kamati maalumu iliyoundwa ikishirikisha taasisi mbalimbali za Serikali kwa lengo la kutengeneza mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji unaojulikana kama Tanzania Electronic Investment Window – TeIW.

Prof. Kahyarara amesema kuwa utengenezwaji wa mfumo huu ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alilolitoa akihitaji Wizara kuanzisha mfumo wa utoaji huduma kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwa na dirisha moja la huduma.

Prof. Kahyarara alieleza kuwa timu hii imeanza kazi hii tangu tarehe 7 Desemba, 2021 ambapo walianza kutengeneza mfumo huu katika awamu ya kwanza na upo katika hatua ya mwisho kukamilika na kuanza majaribio na kwa awamu ya kwanza mfumo umeziweka pamoja taasisi saba ikiwemo NIDA, TRA, BRELA, ARDHI, KAZI, UHAMIAJI na TIC.

Alisema kuwa awamu ya pili ya utengenezwaji wa mfumo huu utahusisha taasisi tano zilizosalia ambazo ni TMDA, OSHA, TANESCO, TBS na NEMC.

“Faida za mfumo huu ni kuwa utasaidia upatikanaji wa vibali vyote vinavyotolewa nchini kupatikana kwa urais na kwa haraka kwani huduma zote zitapatikana kupitia dirisha moja na mwekezaji ataweza kuomba vibali husika mahali popote alipo, pia utasaidia kufuatilia hatua za maombi ya uwekezaji”. Alisema Prof. Kahyarara.

Aliongeza kwa kusema kuwa kuanza kutumika kwa mfumo huu utasaidia kupunguza urasimu, gharama na muda kwani mwekezaji atapata huduma zote kupitia mfumo huu na sio kukutana na watoa huduma na hii itasaidia hata kupunguza rushwa na udanganyifu.

Prof. Kahyarara akatumia fursa hiyo kuwashukuru wabia wa maendeleo Trade Mark East Afrika (TMEA) ambao wamefadhili kuwaweka pamoja wataalamu wa kuandaa mfumo huu na sasa nchi yetu inaenda kunufaika kwani wawekezaji watazidi kuja kwa wingi kwani urasimu utapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa uaandaaji wa mfumo wa dirisha moja kwa wawekezaji (One Stop Centre) Robert John Mtendamema alisema kuwa kituo cha uwekezaji nchini kilianzishwa mwaka 1997 kikiwa na lengo la kuwahudumia wawekezaji kwa haraka chini ya mwamvuli wa dirisha moja (One stop shop) ambapo taasisi mbalimbali za Serikali zinahudumia wawekezaji zimeweka maafisa ambao wana uwezo wa kutoa maamuzi ya kutoa vibali hivyo.

Mtendamema alisema kuwa kupitia mfumo huu unaoundwa sasa utawezesha kuondoa kero mbalimbali kwa wawekezaji hasa zile za kumlazimisha mwekezaji kuingia katika mifumo mbalimbali kutafuta vibali na sasa ataingia katika dirisha moja na kukuta taasisi zote na kufanya maombi kwa wakati mmoja, pia kupitia mfumo huu utawarahisishia wawekezaji kufanya maombi ya vibali na hii itapelekea kuongezeka kwa wawekezaji nchini kwa sababu ya urahisi wa kufanya maombi ya vibali mbalimbali.

Mtendamema aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya TEHAMA kila taasisi ndani ya One Stop Centre wameweza kuwa na mfumo wa kutoa kutoa huduma mbalimbali ambapo mwekezaji anapofika TIC inamuhitaji kuingia katika mifumo isiyopungua 12 ya kila taasisi yenye nywila tofauti kwa ajili ya kufanya maombi.

 

 

Share:

Thursday, December 9, 2021

TFRA YAWASISITIZA WAKULIMA KUACHA DHANA POTOFU MATUMIZI YA MBOLEA YA CHUMVICHUMVI MASHAMBANI

Mkurugenzi mtendaji TFRA  Dkt. Stephen Ngailo. akiwa katika picha na Matlida Kasanga afisa mawasiliano na mahusiano wa TFRA na ofisa udhibiti ubora  Cothal Samwel Kwenye mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi Singida.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo hususani kwa zao la alizeti wakisikiliza mada mbalimbali zikitolewa na wataalamu kutoka TFRA.

Kaimu mkuu wa idara ya kilimo umwagiliaji na ushirika kutoka Halmashauri ya wilaya ya ikungi  Gurisha Msemo akitoa taarifa ya hali ya kilimo katika halmashauri hiyo  wakati wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo.

Mkurugenzi wa TFRA Dkt. Stephen Ngailo akielezea malengo ya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa mikoa ya singida , Dodoma na Tabora .


Na Hamis Hussein - Singida 

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini TFRA imewataka wakulima kila mmoja kuwa balozi katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo ili kuongeza tija kwao binafsi na taifa kwa ujumla .

zaidi ya wakulima 200 kutoka halmashauri ya ikungi wameshiriki mafunzo ya matumizi ya mbolea yaliyoratibiwa na TFRA ambapo mikoa ya Singida , Dodoma na Tabora imepewa kipaumbele kwa kuwa ndio wazalishaji wakuu wa zao la alizeti .

Akizungumza katika mafunzo yao mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt. Stephen Ngailo amesema wao kama mamlaka ya udhibiti wa mbolea kwa kushirikia na wizara ya kilimo na wadau wengine kwa ujumla lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuona mnufaika mwa mwisho wa mbolea aidha muuzaji au mkulima apate tija kulinga na mbolea hiyo ili kuongeza uzalishaji .

"Tunatoa sahihi kwa wakulima, afisa kilimo na wadau wengine kama vile wauzaji wa pembejeo  kuhakikisha ile elimu  iwasaidie kutumia mbolea kwa usahihi , lengo ni kuwa wewe unayetumia mbolea shambani unapata faida , kuwe na tofauti  ya tija kwa wewe ulieweka mbole, kuonyesha kuwa kuweka mbolea inalipa ". alisema Dkt. Ngailo 

Dkt. Ngailo ametumia nafasi hiyo kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni  bora za kilimo ikiwa ni lengo la serikali katika mkakati wake wa kuhakikisha zao la alizeti linazalishwa kwa wingi ili kupunguza uagizaji wa mafuta toka nje ambapo mikoa ya kimkakati ni singida , dodoma na Tabora.

"Mheshimiwa  waziri mkuu alikuja singida kuhamisisha mkakati kuuu ikiwa nia adhma ya kuongeza wa zao la alizeti ili kujitoshereza katika uzalishaji wa mafuta . kuna mikoa ya kimkakati ,  Kuna mkoa wa dodoma niwashuruku wataalamu wetu wametoa mafunzo kama haya , mkoa wa singida na baadaye ni igunga mkoa wa Tabora na haya ndio maeneo yalichaguliwa kuwa ndio wazilishaji  wakuu wa zao la alizeti" . Ameongeza Dkt. Ngailo.

Kaimu mkuu wa idara ya kilimo ushirika na umwagiliaji kutoka halimshauri ya Ikungi Mkoani singida Gurisha Msemo amesema  hali halisi ya matumizi ya mbolea katika halmashauri hiyo bado ipo chini kwa mpaka sasa 5%  ya wakulima ndio wanautumia mbolea ya chumvichumvi.

" Matumizi ya mbolea katika halmashauri ya ikungi ni 5 % asilimia nyingine wanatumia samadi lakini pia kuna familia au wakulima hawatumii kabisa mbolea kwa hiyo sasa baada ya mafunzo haya tunatumaini watakuwa wamepata elimu ya juu ya matumizi ya mbolea". alisema Gurisha 

Baadhi ta washiriki wa washa hiyo  ilikusudia kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea  na kanuni bora zakilimo wamesema dhana potofu iliyopo mtaani ya kuamini kuwa mbolea ya chumvi chumvi inaharibu ardhi ndio sababu kuu ambayo ilikuwa inapelekea wao kutotumia mbolea katika mashamba yao .

Halmashauri ya Ikungi inatarajia kuzalisha tani 72000 za alizeti kutoka kwa wakulima 95000 na kupitia mafunzo hayo tija ya mkulima mmoja mmoja  kama atazingatia kanuni bora za kilimo kama ambavyo mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini TFRA  kiwago za uzalishaji wa mafuta kitakuwa juu sana.

Share:

Thursday, December 2, 2021

NI HATARI ! FUVU LAKUTWA PEMBEZONI MWA BARABARA WANANCHI WASHANGAZWA

 

Na Hamis Hussein - Singida 

Jeshi la polisi mkoa wa singida Limethibitisha  kupatika kwa masalia yanayosadikika kuwa ni ya  binadamu  katika kijiji cha mwankoko mkoani singida 

Mabaki hayo ni pamoja na Fuvu, mifupa, nguo pamoja na nywele 

Jionee mwenyewe hapa.! 



Share:

Sunday, November 28, 2021

SERIKALI YATOA SHILLINGI BILIONI 5.9 UJENZI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 70

 Na Hamis Hussein - Singida

Serikali imetoa shilling bilioni 5.9 kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo mapya ya  hospitali ya rufaa ya mkoa  wa Singida ambayo itarahisisha huduma mbalimbali afya  ikiwemo upasuaji , tiba za kibingwa na  kupunguza gharama za matibabu kwa  wananchi kufuata huduma hizo  hospitali zingine za mbali  kama  Benjamini Dodoma , au muhimbili.



Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr Doroth Gwajima ametembelea kukagua ujenzi huo akiwa kwenye  ziara ya kikazi  na kuridhishwa ujenzi huyo baada ya  kuona umefikia  asilimia 70  ikiwa ni  awamu ya kwanza ya fedha zilizotengwa .

DR. Gwajima alisema kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia  kuruhusu wodi za hospitali ya rufaa ambayo majengo yake  yameshachakaa kuhamishiwa kwenye majengo mapya  ambayo yanajengwa  eneo la mandewa  pamoja na  kurahisisha huduma za afya kwa jamii.

“Kutoka singida nimekuja ziara fupi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali mpya . iliyopo sasahivi ile hospitali iliyopo katikati ya mji imebanwa majengo yake yamepitwa na wakati   , umefika wakati wa kuongeza  kasi ili huduma za rufaa zihamie hospitali mpya ya mandewa  ambayo ni ya kisasa. Serikali  haiko nyuma imeshatenga  na kuleta shilingi bilioni 5.9 . Jengo lote linavyooneka hapa  ni kubwa  kuna sehemu ya upasuaji , maabara na wodi mbalimbali . hii itaruhusu wodi za kule zilizobanana kuhamia huku na  majengo ya hospitali ile yatumike na halmashauri  na hospitali hii itakapo kamilika itatoa nafuu kwa hospitali ya Benjamini mkapa pamoja na gharama za kwenda kutibiwa mbali ”. amesema Dr. Doroth Gwajima.


Wakati akikagua ujenzi wa majengo mapya ya hospitali Waziri Doroth Gwajima ametoa maagizo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida pamoja na watendaji wengine kutoka serikalini kuundwa kwa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha ,  pamoja na dawa ili kuweza kubadilisha na kumaliza matatizo ambayo yamekuwa sugu hususani dawa ambalo limekuwa kama wimbo wa taifa .

Wapo watu wajanja wanaofanya dawa hizi zisifike kwa wagonjwa, utafiti umefanywa  na nyinyi wenyewe, kamati ya dawa iundwe  sio ile kubwa  hii  ni ndogo ya kuhakikisha pale dirishani kwa mfamasia ni wangapi wamepata dawa zote, wangapi wamekosa , lakini katika mifumo yetu ya fedha viko vitengo vinatumia   vifaa tiba vibaya rasilimali  lakini ukiangalia wateja wangapi wamechangia hakuna takwimu , tunataka kamati ya fedha itakayosimamia hayo.

Aliongeza kutaja kamati nyingine ya damu itakayosisimamia uchangiaji wa damu   

Mfumo wa damu salama wananchi wanalalamika   watu wanakosa damu wanashurutishwa wachangie kwanza ndipo wapewe damu nimefika kwenye vituo malalamiko yapo sahihi ni kikundi cha watu wachache wajanja wajanja , lakini wananchi suala lingine  na ninyi hamchangii damu  nimeona hapa kuanzia julai mpaka septemba   asilimia 27 %  ya chupa zilizotakiwa kupatikana asilimi ni ndogo sana lakini je tunashirikishaje mifumo ya wadau waliopo kwenye mkoa huu ili waweze kuhamasisha wananchi kuchagia damu . kamati ya damu iuundwe ili kusimamia hili.




Akizungmza kwa niaba ya  mkuu wa mkoa  , Mkuu wa wilaya Mhandisi Pascas Mulagiri amethibitisha kupokea shilingi bilioni 5.9 ambapo ameanisha kuwa fedha hizo zinatumika katika ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa

“Sisi ni miongoni mwa wanufaika wakubwa mipango ya afya singida tayari tumepokea  bilioni 5.9 katika uendelezaji wa hospitali ya rufaa ya mkoa singida  na ujenzi wake unaendelea na haya  lakini tuna pesa  Bilioni 5.3 kwaajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ambayo yataanza hivi karibuni  haya yakifanyika itakuwa ni mapinduzi makubwa sana katika sekta ya afya hospitali yetu inakuwa  ya rufaa na ukiwa na hospitali hiyo itasaidia kuwa huduma nzuri na kuwa madaktari bingwa” . alisema Mhandisi Mulagiri

Kuhusu changamoto ambayo waliyokuwa nayo halmashauri kukosa hospitali ya wilaya mkuu huyo wa wilaya wa Singida Mhandisi Mulagiri amesema walikosa huduma nyingi ikiwemo madaktari bingwa ngazi ya wilaya.

Suala la kutokuwepo kwa hospitali ya wilaya lilituaathiri  kwa kiasi Fulani ukiangalia katika sekta ya aafya mgawanyo wa huduma za afya , madawa , wahudumu waafya unaendana na kituo hivyo tulikuwa tunakosa mgawanyo wa dawa  na huduma zingine hivyo ujio wa hii nafasi ya kutimia majengo ya hospitali ya general utawasogezea wananchi huduma kuwa karibu.

Mkandarasi wa hospitali ya rufaa ya mkoa  kutoka kambuni ya MCB Justine Kyando amesema kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 70 huku akitoa makadirio ya kumalizika kwa ujenzi huo ili hospitali inaze kuanza kutumika

“Tunashukuru ujio wa mheshimiwa waziri . kwa sasa tumefikia asilimia 70 , kwa sahivi kwa sababu wanataka kutuongezea mkataba  kumaliza hadi ghorofa  tunaweza inaweza kutumia mwaka mmoja na nusu kwa maana hadi mwaka 2023 tunaweza kumaliza ianze kutumika.”


Share:

Saturday, November 27, 2021

ZAIDI YA WAGONJWA 1141 WA VIKOPE WATIBIWA MKOANI SINGIDA

 

Na Hamis Hussein-Singida

Jumla ya kaya 212,952 kati ya walengwa 212812 sawa na asilimia 100.1 % zimefikiwa na mradi wa vikope kutoka shirika la Hellen Keller International ambapo shirika hilo limezitembelea moja kwa moja kaya hizo kuwabaini  wagonjwa wa vikope kisha kuwapatia matibabu ikiwa ni lengo la  kutokomeza ungonjwa huo kwa mkoa wa singida kwani  ni miongoni mwa magonjwa  makuu matano ambayo hayapewi kipaumbele.

Baadhi ya washiriki wa kikao cha kufunga mradi wa vikope mkoani singida wakisikiliza na kujadiliana mambo mbalimbali.

Mradi huyo uliodumu kwa miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake 2019 ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDCP kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ulilenga kupunguza au kuufuta kabisa ungonjwa wa trakoma au vikope ambapo mikoa 20 ikiwemo mkoa wa singida ndiko utekelezaji wake unafanyika ikiwa mradi ambao  unakotekelezwa kupitia shirika la Hellen Keller International kutoka nchini marekani.

 

Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Viktorina Ludovick amelipongeza shirika hilo kwa namna ambayo limeisaidia serikali na jamii katika kutokomeza  ungonjwa wa trakoma alipokuwa akizungumza na washiriki wa kikao cha ufungaji wa mradi huo kumwakilisha katibu tawala wa mkoa.

 

 “Kwa kushirikia na timu zetu za mikoa na halmashauri pamoja na mdau wetu Hellen Keller International tumeweza kutekeleza mpango wa kutokomeza vikope kwa Halmashauri zeto sita  Manyoni , Itigi Ikungi Mkalama Singida Vijijini na Singida Manispaa  jumla 212952 kati ya walengwa 212812 sawa na 100.1% . Hapa tunaona uhitaji ulikuwa mkubwa na tumetekelea mpaka tumevuka lengo”.  amesema Dr Ludovick 

 

Mganga Mkuu mkoa wa singida Dr. Viktorina Ludovick akizungumza na washiriki wa kikao cha kufunga  mradi wa vikope kutoka shirika la HKI katika ukumbi wa Aqua Vitae Resort Singida.


Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kubaini na kutibu wagonjwa wa vikope wataalamu wawili ngazi ya mkoa, wataalamu 13 ngazi ya halmashauri, wahudumu wa afya 1308 ngazi ya kata na vijiji pamoja na wahudumu afya 2851 ngazi ya jamii.

Dr Ludovick ameongeza kuyataja mafanikio kupitia mradi wa vikopte kutoka shirika La Hellen Keller Interentaional kuwa wagonjwa 1141 wa vikope ambao walikuwa na tatizo hilo aidha  bila kujua au  kukosa sehemu ya kupata msaada walipata huduma.

 

Meneja mradi wa trakoma kutoka shirika la Hellen Keller International (HKI) Athuman Tawakal amesema lengo kubwa la kuleta mradi huo ilitokana na takwimu zilizoonyesha uhitaji wa huduma hizo kwa waathirika wa ugonjwa wa vikope.

“ Tumekuja katika maeneo haya  baaada ya kupata takwimu kutoka wizara ya afya kuonyesha ukubwa wa ugonjwa huu wa trakoma  katika maeneo haya na tuliagizwa na wizara kupitia mpango wa kutokomeza magonjwa yasiopewa kipaumbele ili kusaidia halmashauri  na mkoa  katika kuwatafuta wagonjwa na kuwapatia matibabu na tumeweza kufanikiwa . tumeweza kuwasidia watanzania zaidi ya 1100 kuwapatia matibubu na tumekuwa tukifanya ufutiliaji”.

 

Meneja mradi kutoka shirika la HKI Athuman Tawakal Akizungmza na washiriki wakati wa kufunga mradi wa vikope mkoani singida tangu ulipoanzishwa 2019


Dr. Julius Nyenje mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama amelishukuru shirika la HKI kwa kuwajengea uwezo wa mapambano dhidi ya ungonjwa wa trakoma.

“Trakoma au ungonjwa wa vikope ilikuwa moja ya  magonjwa  makuu matano ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele na HKI mmechukua nafasi kubwa sana  na jamii yetu imepata huduma njema .tunawashukuru sana”. alisema dr. Julius mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama.

Mratibu wa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama Dr. Julius Nyenje akitoa shukrani kwa shirika la Hellen Keller International wakati wa kufunga mradi wa vikope .


Fatuma Jumapili, Elizabeth Wilbroad na Shabani Hamisi  ni Baadhi ya wanufaika wa mradi wa vikope kutoka shirika la HKI wamesema huduma ya matibabu ya vikope imewasaidia sanaa kurejesha uwezo wao wa kuona na kulipongeza shirika hilo kwa namna lilivyotekeleza mradi huo.

 

Dr Upendo Mwakabalile mratibu wa huduma za macho mkoa wa singida amewasisitiza wataalamu wengine waliopata mafunzo ya namna ya kuwahudumia  wagonjwa wa vikope kutunza takwimu ili ziweze kusaidia baaadae na kuwataka elimu waliopata kuifanyia kazi kwa watu wengine wenye uhitaji.


“Naomba kila mtu azingatie sana kwa sababu pasipotakwimu kazi yetu tulioifanya kwa miaka mitatu itakuwa imepotea, kwahiyo takwimu inakuwa ni ushahidi. hawa wahudumu 13 tuliopewa mafunzo tusipofanyia kazi hiyo elimu yetu itakuwa sawa na bure”.  
amesema Dr. upendo

Mradi wa vipoke mkoani singida umetekelezwa na shirika la Hellen Keller International ikiwa ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya  maendeleo ya jamii  jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa  taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDCP kwa kushirikiana na timu za mikoa na wilaya  na wadau mbalimbali ambapo mradi umetekelezwa kwenye wilaya sita ambazo  ni manyoni , itigi , ikungi ,mkalama , singida manispaa na singida  vijijini  ambazo ziliathiliwa na ungojwa wa vipoke kwa kiwango kikubwa .





 

 

Share:

Thursday, November 25, 2021

CHIFU NDOVU SENGE ASIMIKWA KUWA CHIFU MKUU SINGIDA

 Na Hamis Hussein -SINGIDA


Umoja wa machifu mkoa wa singida umewaomba wanaumoja huo kufanya zoezi la kuwasimika machifu wengine katika maeneo yao kabla ya kwenda kushiriki mkutano mkuu wa machifu Tanzania  utakaofanyika mkoani Kilimanjaro katika kujiandaa kukutana na mkuu wa machifu Tanzania  chifu hangaya  ambaye ni rais wa awamu ya sita mh. Samia suluhu hasani.

Akizungumza wakati wa kumsimika mkuu wa machifu mkoa wa singida chifu  Mugenyi Senge Mugenyi Ndovu , mwenyekiti wa umoja wa machifu mkoa wa singida   Chifu  Mjengi Gwau amewataka  kushirikiana ili kutimiza malengo huku akitoa rai ya kuundwa kwa mabaraza ya wazee watakaosimamia mila na desturi za kitemi
" Na wengine wote tusaidiane wafanye haya , tunangojwa kwenda kufanya mkutano umoja wa machifu tannzania  moshi marangu ili tuchague viongozi wa umoja wa machifu , tushamaliza chifu Hangaya anatuita machifu wote dodoma ..... halafu tutaunda mabaraza ya wazee yatakayosimamia  mila na destiri zetu" amesema Chifu Mjengi .
Baada ya kusimikwaa kuwa mkuu wa machifu mkoa wa singida chifu mugenyi senge mugenye ndovu ameshukuru kupata nafasi hiyo na kueleza kuwa atakuwa ni kiunganishi kati ya serikali na jamii katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaendeleo
"Mimi nimefurahi sana kwa kutawadhwa kuwa chifu , kuna miradi mingi sana ambayo serikali imekuwa ikitoa  lakini wananchi stahiki wanazotakiwa  kupata walikuwa hawapati kwa sababu hakukuwa na mtu wa kuwatetea ....... imekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwatetea kwasababu nawajua raia  .... mimi nitakuwa kiunganishi kati ya serikali na jamiii." amesema chifu Mghenyi Senge Ndovu.

Kuhusu migogoro ya ardhi chifu huyo ameeleza namna ambavyo umilikishaji usiohalali unavyopelekea migogoro na kuiomba serikali kushirikiana
 katika kuitatua huku akitoa shukurani kwa  mkuu wa machifu Tanzania  chifu hangaya  rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  samia suluhu Hassan
" Kuna baadhi ya watu ambao wametoka katika mikoa mingine wametumia njia za ujanja ujanja kumiliki  maeneo makubwa ya ardhi .... sisi tutasimama kuhakikisha wananchi wanapata haki zao.kwanza nimpongeze chifu hanya , wakatai anasimikwa kuwa mkuu wa machifu tanzania nilikuwa miongoni mwa machifu niliokuepo kwenye tukio  hilo  na hii  inaonesha utamaduni na mila zetu zinaheshimika . ameongeza chifu Mghenyi Senge Ndovu.

Katibu wa chifu ndovu amabaye pia ni mtoto wake salum mghenyi ndovu amesema mkuu huyo wa machifu atasimamia maeneo ya asili kama vile misitu na vyanzo vya maji
" kuna mambo mengi sana ambayo chifu atayasimamia zamani tulikuwa na maeneo yetu ya asili kama vile msitu , vyanzo vya maji ambayo kwa sasa havizingatiwi sana  kuna maagizo alitoa katibu wa wizara ya sanaa utamaduni dkt. hassani abasi kuwa machifu waorodheshe maeneo yao yalikuwa yakiutawala wa kichifu... hivyo kuna maeneo hapa singida yanahitaji usimamizi wa chifu na ndio kazi ambayo ataifanya .  amesema salum mghenyi  Ndovu katibu wa chifu Mghenyi senge Ndovu.

Mkoa wa singida una jumla ya machifu sita ambao huongoza shughuli mbalibali za kitemi kama mila na desturi ya jamii yao.



Share:

Thursday, November 29, 2018

Wednesday, November 28, 2018

Majaliwa aanza na wanaotuhumiwa kutafuna mabilioni ya fedha wilayani Nyang'hwale

Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Share:

Tuesday, November 27, 2018

RC Geita mbele ya Waziri Mkuu “nafuu tukikagua tukute mtu kajinyonga”

Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akitoa salamu za shukrani na kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) aliyeanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita jana, kulia ni mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani.
Share:

Sunday, November 25, 2018

Biteko atoa maamuzi kilio cha wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Kahama

Na George Binagi-GB Pazzo 
Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo ya Bushimangila yaliyopo Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa kutoa idhini kwa wachimbaji hao kuendelea na shughuli za uchimbaji katika machimbo hayo.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alitoa idhini hiyo jana baada ya kufanya ziara katika machimbo hayo ya Bushimangila kwa lengo la kukagua shughuli za uchimbaji, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wadogo wa dhahabu.
Share:

Monday, November 12, 2018

Solomon Mkubwa akonga nyoyo za wakazi wa Mwanza, RC Mongella afurahia

Mwimbaji wa muziki wa Injili, Solomon Mkubwa akitumbuiza kwenye uzinduzi wa albamu ya Injili ya “Jerusalem Band” kutoka kanisa la EAGT Kiloleli chini ya Mchungaji Dkt. Jacob Mutashi, uliofanyika Belmont Fairmont Hotel Jijini Mwanza, Novemba 11, 2018. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella.
Tazama Video hapa chini
Na George Binagi-GB Pazzo
Share:

Uzinduzi wa Albamu ya Jerusalem Band wafana Jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa albamu ya kwaya ya "Jerusalem Band" kutoka Kanisa la EAGT Kiloleli lililopo Manispaa ya Ilemela chini ya Mchungaji Mwl. Dkt. Jacob Mutashi (kushoto). Uzinduzi huo ulifanyika jana Novemba 11, 2018 katika ukumbi wa Belmont Fairmont Hotel Jijini Mwanza.
Share:

Friday, November 9, 2018

Tuesday, August 23, 2016

DC STAKI ATENGA SIKU YA JUMATATU KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO



Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki shughuli za maendeleo kwa kufyeka baadhi ya vichaka

 Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya



Dc Senyamule akishiriki zoezi la kupanga matofali yaliyofyatuliwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani humo.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga Siku moja katika Juma ili kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.

Share:

Monday, August 22, 2016

Namba za Simu za Utoaji Wa Malalamiko Na Kero Juu Ya Huduma Za Afya Nchini

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007)
Share:

Saturday, August 20, 2016

Jela miaka 30 Kwa Kumbaka Mwanafunzi wa Miaka 9

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Urambo mkoani Tabora, imemuhukumu Deus Barnaba(45) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka tisa.

Akitoa hukumu hiyo mwishoni wa wiki iliyopita, Hakimu Mkazi, Baptista Kashusha, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka hivyo kumuona mshitakiwa ana hatia.
Share:
Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com