METDO Tanzania

METDO Tanzania
Showing posts with label Michezo kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Michezo kitaifa. Show all posts

Tuesday, August 23, 2016

FIFA yaiongezea ujuzi Tanzania wa makocha


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine limeipa nafasi Tanzania kwa kutoa kozi maalumu ya stamina (Physical fitness) kwa makocha wa Tanzania wenye leseni kiwango B inayoanza leo Agosti 22, 2016. Kozi hiyo inayoendeshwa na mkufunzi kutoka FIFA, Dk. Praddit Dutta, raia wa India itafikia ukomo Ijumaa wiki hii.
Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliishukuru FIFA kwa namna inavyoipa nafasi Tanzania katika kozi mbalimbali hususani za ukocha na uamuzi.
“Si kila nchi inapata privilege (fursa) kama hii. Bila shaka FIFA inatambua uwezo wa makocha wa Tanzania kwa sasa. Mjue kuwa FIFA ina watu wa kuwapa taarifa kila kona. Kama mngekuwa mnafanya vibaya, FIFA wangesema Tanzania bado, kwa hiyo kozi zisipelekwe… lakini inaonekana mnafanya vema, mngefanya vibaya msingefikiriwa,” alisema Mwesigwa aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo.
Mwesigwa amesema kwa kuwa FIFA ina malengo chanya na Tanzania kwa kutoa kozi mbalimbali ikiwamo hiyo ya physical fitness inayolenga kuwapa ujuzi makocha hao kuwajengea uwezo wachezaji kuwa na stamina.
Hivyo akawataka makocha wanaohudhuria kozi hiyo kutumia fursa hiyo ya mafunzo si kwa ajili yao peke yao bali kuendeleza ujuzi huo kwa wengine ambao hawakubahatika kuwa sehemu ya wateule wa FIFA.
Naye, Mkufunzi wa kozi hiyo, Dk. Dutta alisema: “Bila shaka Tanzania inakwenda kufungua ukurasa mwingine wa soka la weledi kwa kuwa na wataalamu mbalimbali katika ukocha na uamuzi. Mnachotakiwa ni kujitahidi kufanya vema na kozi nyingine nyingi zinakuja.”
FIFA kwa kushirikiana na Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mkurugenzi Salum Madadi, imepitisha majina ya makocha 27 kuhudhuria kozi hiyo inayofanyika katika Hosteli ya TFF iliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Makocha wanashiriki kozi hiyo ni Mohammed Muza, Samwel Moja, Nassa Mohammed, Jemedari Said, Oscar Mirambo, Wane Mkisi, Cletus Mutauyawa, Shaweji Nawanda, Kizito Mbano, Dennis Kitambi, Sebastian Nkoma, Fikiri Mahiza, Nyamtimba Muga, Nassor Mwinchui, Alfred Itaeli, Henry Ngondo, John Tamba, Kidao Wilfred, Luhaga Makunja, Mohammed Tajdin, Mohammed Silima, Salum Ali Haji, James Joseph, Kessy Mziray, Daudi Sichinga, Bakari Shime na Salum Mayanga.
Share:

TFF YAPIGA PINI WACHEZAJI WALIOSAJILIWA ‘KIMAGUMASHI’

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kutoa tahadhali kwa timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) juu ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wanamatatizo kwenye usajili wao.
Majimaji ya Songea
Mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili. Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.
Mwadui FC ya Shinyanga
Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili Mwadui FC ilihali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda. Mwadui isimtumie mchezaji huyo.
Mbeya City ya Mbeya
Mchezaji Saidi Mkopi, pia amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kujisali timu mbili. Imebainika kuwa akiwa bado na mkataba na Tanzania Prisons ya Mbeya hivyo Mbeya City isi1mtumie mchezaji huyo.
African Lyon ya Dar es Salaam
Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon ya Dar es Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa African Lyon kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya Agosti 27, 2016. African Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.
Mbao FC ya Mwanza
Mchezaji Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam, kabla ya Agosti 27, 2016. Mbao FC isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.

Share:

MECHI 15 MFULULIZO PASIPO KUPOTEZA, RUVU SHOOTING WANAWEZA KUSHANGAZA MSIMU HUU?


KABLA ya mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Mtibwa Sugar huko Manungu Complex, Turiani, Morogoro, ofisa habari wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani, Masau Bwire alipost picha katika akaunti yake ya facebook ‘akila muwa.’
Shooting ilikuwa ikicheza game yake ya kwanza baada ya kurejea ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa. Bwire mtu mwenye kupenda utani na mwenye kupendelea kuisifia sana timu yake, aliandika pia katika picha yake hiyo: “Tutawatafuna kwa staili hii Mtibwa Sugar hapa Manungu Complex leo August 20, 2016,” na ndicho kilichokuja kutokea baada ya dakika 90.’
Wameendeleza rekodi ya kupoteza mchezo wowote, kati ya 15 waliyokwisha cheza. Hawakupoteza katika game zao zote za ligi daraja la kwanza msimu waliopita, na bao la mkwaju wa faulo la kiungo ‘maestro’ siku ya Jumamosi iliyopita lilitosha kuwapa ushindi wa kwanza katika VPL tena wakicheza ugenini dhidi ya mabingwa wa miaka ya 1999 na 2000, timu ya Mtibwa Sugar.
Shooting imeendelea kucheza mechi za ligi za juu Tanzania Bara pasipo kupoteza. Mechi 15 mfululizo pasipo kupoteza, Ruvu Shooting wanaweza kushangaza msimu huu?.
Share:
Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com