Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi hiyo hafla hiyo
ilifanyika katika Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa
jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni
Mwenyekiti Baraza la Wafanyakazi akizungumza katika uzinduzi wa Baraza
jipya la wafanyakazi wa taasisi hiyo hafla hiyo ilifanyika katika
Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Katibu TUGHE mkoa wa Dodoma akimshukuru
mgeni rasmi (hayupo pichani)baada ya kuwazindulia Baraza jipya la
wafanyakazi wa taasisi hiyo hafla hiyo ilifanyika katika Taasisi ya
Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Sehemu ya Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa wakifuatilia uzinduzi wa baraza hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ambaye alikuwa mgeni
rasmi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza Jipya la wafanyakazi wa
taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (katikati) akiangalia
kitabu cha muongoza mara baada ya kuzindua Baraza Jipya la wafanyakazi
wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi cheti
Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi
Dkt.Alphonce Chandika baada ya kuzinduliwa kwa Baraza Jipya la
wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini
Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi cheti Afisa
Utumishi-Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Muadhi Mayunga baada ya
kuzinduliwa kwa Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya
Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi cheti Kaimu
Mwenyekiti wa TUGHE Hospitali ya Benjamini Mkapa,Benjamini Babere baada
ya kuzinduliwa kwa Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali
ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula(katikati) waliokaa
akiwa katika picha ya pamoja na watendaji mara baada kuzindua Baraza
Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa
jijini Dodma.
……………….
Na.Alex Mathias,Dodoma.
TAASISI ya Hospitali ya Rufaa ya
Benjamin Mkapa imeunda na kuzindua Baraza jipya la wafanyakazi wa
taasisi hiyo, ambalo limeundwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa
hospitali hiyo, ambayo ni miongoni mwa hospitali kubwa hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza
hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Dkt. Zainab Chaula, amewataka wafanya kazi wa taasisi hiyo
kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma sambamba na kuwa wazalendo, na
kuwajali wagojwa.
Dkt Chaula amesema kazi ya utabibu na
udaktari ni ya neema na Rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na inayohitaji
kuwa na uvumilivu , huruma na maneno ya Faraja kwa Wagonjwa hivyo kila
Mmoja anatakiwa kuguswa pindi anapotoa huduma kwa mgonjwa.
“Tunajifunza kila siku,kwa hiyo nyie
mlioteuliwa mtuwezeshe,haki haipo bila wajibu,na kila mmoja akijituma
atatizimiza wajibu wake,mimi sikumbuki kutumwa na napata shida kum-push
mtu,na lazima tutengeneze Mechanism ya watu kufanyakazi bila kutumwa”
“Hakuna kazi ya neema na ibada tunayo
fanya kama hii,Mtu ana Stress zake,ana shida,hana hela lakini
unamfariji,unamtibu,mwisho wa kazi saa 9 ukifanya kazi mpaka saa 11 au
saa 1 jioni una dhambi gani.”Amesema Dkt Zainabu.
Mwa upande mwingine, Dkt Chaula amewataka
wafanyakazi kuwa Wepesi katika kutekeleza Majukumu yao na kutowakwaza
wagonjwa na wananchi kwa ujumla hivyo ni jambo la busara kupeana Moyo
katika kazi ngumu na yenye wito ya utabibu na kumtegemea Mungu katika
changamoto wanazokumbana nazo .
“Kwa makusudi tu mtu anakuja halafu
anatoka analia ofisini kwako unajisikiaje,lazima tupendane tuhurumiane
tukitengeneza system ya namna hii katika maisha yetu tutakuwa na
marafiki wengi kuliko maadui,tusameheane” Amesema.
Kwa upande wake Katibu wa Baraza la
wafanyakazi mkoa wa Dodoma,ambaye pia Mjumbe Taifa wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali kanisa la Waadventista Wasabato ,[ATAPE]
Bw.Mchenya John, amesema wataendelea kuyafanyia kazi na maelekezo yote
muhimu yaliyotolewa.
Na kuzungumzia namna walivyofanya
mchakato wa uanzishaji wa Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na Hospitali ya
Rufaa ya Benjamin Mkapa akitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa awamu ya
nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha uanzishaji wa Hospitali
hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi
Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ambaye pia mkurugenzi
mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt Alphonce Chandika amesema taasisi hiyo
ina takriban miaka mitatu tangu ianzishwe.
Na amebainisha kuwa walikuwa hawajaunda
Baraza la Wafanyakazi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na
wafanyakazi kutokujitosheleza lakini kwa sasa idadi imejitosheleza na
wameona kuwa na umuhimu wa kuwa na Baraza ambapo tayari na katiba na
mkataba wa Baraza hilo ilishatengenezwa.
0 comments:
Post a Comment