Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
akikabidhi hundi kwa moja ya kikundi cha walemavu wa ngozi katika hafla
fupi ya kukabidhi mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vya vijana,
wanawake na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya
Sumbawanga
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
akikabidhi hundi kwa moja ya kikundi cha walemavu wa ngozi katika hafla
fupi ya kukabidhi mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vya vijana,
wanawake na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya
Sumbawanga
……………………..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
ameisifu Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuzidisha kiwango
cha asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, akina Mama na Watu wenye Ulemavu
kwa kutoa shilingi 253,228,000/= zaidi ya lengo la awali ambapo
halmashauri ilitakiwa kutoa Shilingi 2,212,104,000/= kutokana na makisio
ya makusanyo yake ya ndani yaliyolenga kukusanya Shilingi
2,212,104,000/=.
Mh. Wangabo alisema kuwa kiwango hicho
cha asilimia 10 ambachoo Manispaa ya Sumbawanga wameweza kukitoa ni sawa
na asilimia 115 kutokana na mapato yaliyokusanywa ya shilingi Bilioni
3.1 ambayo ni tofauti na makadirio yaliyofanyika kwa mwaka wa fedha
2018/2019.
“Taarifa ya Mkurugenzi imeonesha kuwa
kuna mafanikio ya kujivunia katika suala zima la uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi kwa kipindi cha Miaka sita, kiwango cha fedha kinachotolewa
kama mtaji kwa wajasiriamali kimekuwa kikiongezeka kila Mwaka na kwa
Mwaka huu wa fedha 2018/2019 Manispaa imevunja rekodi kwa kutoa Shilingi
253, 228,000/= jambo hili ni la kupongezwa kwa mafanikio mliyofikia ya
kutoa fedha 10% ya mapato ya ndani kwa 115% haya ni mafanikio makubwa
sana, hivyo Hongereni sana Manispaa ya Sumbawanga,” Alisema.
Aidha, aliupongeza uongozi mzima wa
Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Halmashauri hiyo kwa kutekeleza sheria ya
fedha ya mwaka 2018 inayoelekeza utekelezaji wa uwezeshaji wa vijana,
kinamama na watu wenye ulemavu na kuzitaka halmashauri nyingine za mkoa
kuiga mfano huo na hatimae kuwafaidisha wananchi kwa mikopo isiyo na
riba ili waweze kujiinua kiuchumi.
Wakati akisoma taarifa ya utoaji wa
mikopo Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisema
kuwa siku ya leo (28.6.2019) Halmashauri itatoa mikopo kwa vikundi 32
ambapo kati ya hivyo vikundi vya Wanawake 13, Vijana 14 na Watu wenye
Ulemavu 5 ambapo kiasi cha Tsh. 73,678,000 kitatolewa kama uwezeshaji wa
Wananchi.
“Kwa maana hiyo, Halmashauri ya Manispaa
ya Sumbawanga kwa kipindi cha mwaka 2018/19 itakuwa imeweza kutoa mikopo
kwa vikundi 114 vikiwemo vya Wanawake 56, Vijana 44 na watu wenye
ulemavu 14 Ambapo kiasi cha jumla ya Tshs. 253,228,000.00 zitakuwa
zimetolewa kwa makundi yaliyoainishwa. Hivyo itapelekea kufikiwa kwa
jumla ya wanachama 1,135 kama wanufaika wa mikopo hiyo kwa mwaka wa
fedha 2018/2019,” Alieleza.
Pamoja na mafanikio hayo makubwa,
Mtalitinya hakusita kugusia changamoto ambazo halmashauri inakumbana
nazo ikiwemo Hamasa ndogo ya uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi, Uelewa
mdogo wa Jamii kuhusu uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi, Uelewa mdogo
wa fursa za kiuchumi kwa Jamii. Kukosekana kwa masoko ya bidhaa za
vikundi. Na hivyo kuahdi kuendela kutoa elimu ya ujasiriamali kwa
vikundi ngazi ya kata na mitaa.
Katika hatua nyingine Mh. Wangabo
alichukua fursa hiyo kukabidi kikombe cha ushindi wa jumla wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2018 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga iliibuka na ushindi huo.
0 comments:
Post a Comment