
************************
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika
halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero kwa tuhuma za ubadhilifu wa
fedha zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.
Mbali
na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi
hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake
ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Reina Mrema ambaye anadaiwa
kuchukua kiasi cha sh. milioni 298, Haile Njitango milioni 73, Linus
Mdembo kiasi cha sh. milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa
Kata.
Waziri
Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao leo (Jumapili, Septemba 15,
2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero
pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku
ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.
Kuhusu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane ambaye
aliingiziwa sh. milioni tano katika akaunti yake binafsi, Waziri Mkuu
ameagiza azirudishe mara moja na amkabidhi stakabadhi ya kuonesha kuwa
amerejesha fedha hizo kabla hajamaliza ziara yake mkoani hapa.
Amesema
“Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha
zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida,
hatutavumilia.”
Waziri
Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali
(CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa
Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa
bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni
727 hazijulikani zilipoenda.
Amesema
katika mitambo kumi ya ukusanyaji wa mapato iliokaguliwa imeonyesha
kiasi cha shilingi milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa bank na
hivyo kuishia mikononi mwa watu.
Waziri
Mkuu amesema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa fedha hizo
ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halamshauri
hizo kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara
aitwaye Gregory Midas.
Hata
hivyo Waziri Mkuu ameagiza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika
halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo
na ubadhilifu wa fedha hizo na badae kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini
mara moja na asibugudhiwe.
“Mlimsimamisha kazi kwa sababu mlijua amegundua madudu yenu, lakini haisaidi, arejeshwe kazini naagiza apewe ulizi wakutosha.”
Kwa
upande wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Waziri Mkuu
amesema zaidi ya sh. milioni 600 hazijulikani zilipo huku kiasi cha
shilingi milioni 98.5 zikidaiwa kuingizwa katika akaunti za watumishi wa
halamshauri hiyo bila maelezo yeyote.
0 comments:
Post a Comment