Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tawi la SOKOINE CBE leo wamejitokeza na kufanyaa usafi katika kitu cha Afya Buzuruga, ilikiwa Lengo ni kuwawezesha vijana kujijengea uwezo wa kuweza kushiriki shughuli za kijamii na kutengeneza mwamko wa kuona kua wao wana jukumu la kuhakikisha kuwa wanakuwa kiigizo chema katika jamii.
Usafi huoo uliambatana na zoezi la utoaji msaada kwenye wodi ya akina mama na watoto pia na kwa wagonjwa wengine walio lazwa hospitali hapo.
Sambamba na hilo pia wasomi hao waliweza kupima afya zao(HIV). hili lilikuwa ni kuonesha umuhimu wa kuweza kujua hali za afya zao na kuwa kielelezo kwa jamii kwa kuwaonyesha wananchi umuhimu wa kujua afya zao.
Akizungumza na wanachuo hawa wa CBE mganga mfawidhi wa Dkt. Mange aliwashukuru kwa kuweza kuja kufanya usafi katika kituo hicho kwan mara kadhaa wamekuwa wakielemewa katika kuhakikisha usafi unafanyika kwa muda kutokana na uhaba wa vifaa na wafanyakazi.
Pia ameishukuru serikali kwa ajili ya fedha mln 400 za mradi wa majengo ili kuwezesha urahisishaji wa huduma kwa wananchi. Lakini kuweza kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika mwaka huu.
Suala la kujitolea kufanya usafi katika maeneo ya hospitali limekuwa likufanywa na vikundi vichache katika jamii,ukilinganisha na kwamba bado maeneo hayo yanahitaji uwepo wa wananchi wanaojitolea,licha ya hilo wagonjwa waliopo hospitali wanahitaji faraja kutoka kwa wanajamii panapopatikana kikundi au vikundi vya kwenda kuwaona ni vyema.
0 comments:
Post a Comment