NAIBU wa waziri wa Kilimo Omary
Mgumba amesikitishwa na kutotekelezwa katika kiwango kinachotakiwa Mradi wa
umwagiliaji wa Tulo Kongwa katika halmashauri ya Wilaya ya Morogoro licha
ya serikali kuwekeza fedha nyingi katika Maradi huo.
Mgumba ametoa kauli hiyo wakati wa
ziara yake ya kukagua miradi ya umwagiliaji, kuhamasisha kilimo cha Pamba
pamoja umuhimu wa Kujiunga katika vyama vya ushirika katika wilaya ya Morogoro.
Katika ziara hiyo Naibu waziri wa
Kilimo aliambatana na Mkurugenzi Mkuu bodi ya Pamba, Marco Mtunga na mrajisi
wa vyama vya ushirika Tito Haule pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa
Morogoro.
Mgumba amesema kuwa licha ya mradi
huo kugharimu fedha nyingi za serikali lakini usimamizi wake ulikuwa mbovu kwa
baadhi ya viongozi hali iliyofanya kutekelezwa chini kiwango.
Hata hivyo naibu waziri Omary Mgumba
amesema kuwa Mradi wa Umwagiliaji Tulo Kongwa utatumika katika zaidi ya
hekta 5,000.
Pia amewataka wananchi wanufaikka na
Mradi huo kujikita katika kilimo cha kisasa ili kuweza kuvuna mavuno yenye tija
kwa maendeleo ya taifa naya kwao binafsi,kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo.
Awali wananchi hao katika risala ya
katibu wa umoja wa wakulima wa umwagiliaji wa Tulo/Kongwa walimueleza naibu
waziri wa Kilimo kuwa toka kuanza kwa kilimo cha umwagilijo wameweza kuongeza
uzalishaji kutoka gunia 3 kwa heka 1 hadi kufikia gunia 20.
Aidha wameiomba serikaliya Halmashuri
hiyo kwa kushirikiana na TARURA kutengeneza barabara ili kuwawezesha
kusafirisha mazao yao vizuri sambamba na kupelekewa huduma ya umeme ili kuweza
kuunguza mchele badala ya Mpunga kama wanavyofanya hivi sasa.
Awali akiwa katika eneo la Matombo
Naibu waziri wa Kilimo amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuwa na nidhamu
katika matumizi ya fedha ilikuweza kujenga imani kwa wanachama wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu bodi
ya Pamba,Marco Mtunga ametumia fursa hiyo kuwataka wakulima ndani ya
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kujikita katika kilimo cha Pamba kutokana na
kuwa na faida kubwa huku pia likiwa ni zao lenye kuvumilia ukame.
Nae
mrajisi wa vyama vya ushirika Tito Haule ameeleza kuwa
vyama vya ushirika vina faida kubwa ikiwemo kumlinda mkulima kwa kumuepusha na
walanguzi wa mazao ambao umekuwa ukipelekea mkulima kurudi nyuma kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment