Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula wakati wa Semina ya Wabunge hao iliyohusu Sekta ya Nishati iliyofanyika jijini Dodoma.
Watendaji mbalimbali kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi hizo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa wakati wa semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyohusu Sekta ya Nishati.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa kuhusu Sekta ya Nishati katika Semina ya Wajumbe hao iliyofanyika jijini Dodoma.
Serikali
imesema iko katika hatua za awali za kuandaa mpango wa uagizaji wa
gesi ya mitungi (LPG) kwa pamoja kama ilivyo kwa mafuta ya Petroli hali
itakayosaidia kudhibiti masuala mbalimbali ikiwemo bei ya gesi hiyo
.
Akizungumza
wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
iliyofanyika jijini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alisema kuwa
dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, wananchi katika maeneo yote nchini
wanafikiwa na huduma hiyo, hivyo Serikali itaratibu usambazaji wa gesi hiyo
badala ya kuwaachia wauzaji wenyewe kuamua maeneo wanayotaka
kupeleka gesi.
‘’
Serikali ikitangaza bei elekezi kulingana na soko, itawafanya wauzaji wafuate
bei hiyo badala ya wao kujipangia, hii itasaidia wananchi kuuziwa gesi kwa
gharama inayofanana katika maeneo mbalimbali ambapo gesi hiyo itauzwa.”alisema
Dkt. Kalemani.
Alieleza
kuwa, suala la sasa la kila muuzaji kujiamulia sehemu anayotaka kupeleka gesi
inafanya maeneo mengine kukosa kabisa nishati hiyo hivyo sasa Serikali itaweza
kuwadhibiti wauzaji na kuhakikisha kuwa maeneo yote nchini yanafikishiwa gesi.
Aliongeza
kuwa, utaratibu wa kuagiza gesi inayotumika majumbani kwa pamoja
utasaidia Taifa kutambua kiwango halisi cha gesi kinachohitajika nchini na
kiasi cha gesi kinachoingizwa nchini na hivyo kusaidia pia katika shughuli za
ukusanyaji wa mapato.
Awali,
akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto
Simon alisema kuwa, Wakala huo kwa sasa unafanya tathmini ya namna
bora ya kuanza uagizaji wa pamoja wa gesi ya mitungi (LPG) kwa kuzingatia maoni
kutoka kwa wadau mbalimbali.
Akizungumzia
faida mbalimbali zinazotokana na uagizaji wa mafuta wa pamoja, Simon alisema
kuwa, ni kuweka mazingira sawa ya kibiashara kwani gharama za uagizaji wa
mafuta ziko sawa kwa makampuni yote na kuondoa mianya ya rushwa katika uagizaji
wa mafuta kwani ufunguzi wa zabuni hufanyika kwa uwazi na washiriki wote
huridhika na matokeo ya zabuni.
Alitaja
faida nyingine kuwa ni, Taifa kuwa na uhakika wa usalama wa upatikanaji wa
mafuta kwa muda wote na kuwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za mafuta
zinazosaidia katika ukusanyaji wa mapato na kupanga bei elekezi ya mafuta.
Aliongeza
kuwa, mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umewezesha nchi kudhibiti ubora wa
mafuta yanayoingia nchini na pia kuongezeka kwa sehemu za kupokelea mafuta
kama bandari ya Tanga na Mtwara, tofauti na ilivyokuwa awali kwani
Bandari ya Dar es Salaam ndiyo ilikuwa ikitumika kwa shughuli hizo.
Kutokana
na hilo, alisema kuwa, nchi mbalimbali barani Afrika kama vile Malawi, Zambia
na Msumbiji wamekuja kujifunza kuhusu mfumo huo wa uagizaji mafuta
ili waweze kuutumia katika nchi zao.
0 comments:
Post a Comment