BMG Habari
Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afya (MISA) tawi la Tanzania kupitia ufadhili
wa taasisi ya FESI Media Africa, imeandaa mafunzo ya siku tatu kuanzia leo
Machi 14, 2019 kwa Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi.
Mafunzo
hayo yaliyowashirikisha Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo, Watunza Kumbukumbu,
Makatibu Muhtasi, Walinzi pamoja na Wahudumu wa Mapokezi mahakamani yamelenga
kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuboresha huduma kwa wateja na haki ya kupata
taarifa.
Akifungua
mafunzo hayo, Kaimu Jaji Mfawidhi, Mhe. Patricia Fikirini amesema yatasaidia
kuleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma na taarifa kutoka idara
mbalimbali za Mahakama.
Naye
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomary alisema pamoja na mambo mengine,
pia washiriki wa mafunzo hayo watajifunza jinsi ya kutoa taarifa na kuomba
taarifa, ujuzi wa misingi na sifa za kushughulikia malalamiko, manufaa ya kushughulikia
malalamiko kwa wakati, jinsi ya kuwahudumia wateja.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya MISA tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa
amebainisha kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mpango wa muda mrefu kati ya
taasisi hiyo na muhimili wa Mahakama katika kuboresha huduma kwa wateja pamoja
na utoaji wa taarifa kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi MISA Tanzania, Sengiyumvya Gasirigwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi MISA Tanzania, Sengiyumvya Gasirigwa akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo.
Mgeni rasmi, Kaimu Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Patricia Fikirini akifungua mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo hayo.
Mwezeshaji, Wakili James Malenga pamoja na washiriki wengine wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania, Salome Kitomari (kulia), akisalimiana na mgeni rasmi Kaimu Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Mhe. Patricia Fikirini
0 comments:
Post a Comment