Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku saba kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, kuhakikisha anaunda timu ya uchunguzi ili kuwabaini wadaiwa wa shilingi bilioni 1.34 za makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri na kuwachukulia hatua wahusika wote ili kuleta ustawi katika utekelezaji wa majukumu ya kiserikali.
Amesema hayo baada ya kupitia taarifa za makusanyo
na kubaini tatizo la kutowasilishwa kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa
kutumia mfumo wa Local Governent Revenue Collection Information System (LGRCIS)
na kueleza kuwa kumekuwa na watendaji ambao sio waaminifu wanaokabidhiwa
makusanyo hayo na kuyaingiza kwenye matumizi binafsi wakitegemea
kurudisha na matokeo yake Bili za wakusanyaji hazikubali kutoka kwenye mfumo
hadi fedha zote alizokusanya zitimie.
Akitolea mfano halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mh.
Wangabo alisema kuwa “hadi kufikia mwezi Februari mwaka 2019, jumla yaShilingi
Milioni 98 zimetumika kama sehemu ya gharama za wakusanyaji baada ya kuzikata
na kutumia. Matokeo yake fedha zinapelekwa Halmashauri zikiwa pungufu na
kuongeza kuwa jumla ya shilingi 241 za halmashauri hiyo zilitumika kabla ya
kupelekwa benki jambo hilo ni kinyume na kifungu cha 32 cha Memoranda ya Fedha
za Serikali za Mitaa.”
Alitoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa semina ya
mafunzo elekezi kwa waheshimiwa madiwani kutoka katika halmashauri zote nne za
Mkoa wa Rukwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo Mh.
Wangabo alikuwa mgeni rasmi wa semina hiyo.
Akitoa neno la Shukurani kwa mgeni rasmi mstahiki
Meya wa manispaa ya Sumbawanga alipongeza juhudi za mkuu wa mkoa wa Rukwa
kuhakikisha anasimamia vyema maendeleo ya mkoa huo, na kumuhakikishia kuwa
hawatamuangusha katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka
“ Sisi kama ALAT mkoa na nipende kuwaarifu madiwani
wa halmashauri zote na itakuja kwenye vikao vyenu, tuliona kuliko kulalamika
kwa kusema hatuna vyanzo vya mapato, halmashauri za mkoa wa Rukwa zina migogoro
mingi ya ardhi kwa kutopanga matumizi ya ardhi, hivyo tumeamua ardhi zote ndani
ya mkoa zipimwe na tumeshanunua mashine ya Alat K yenye thamani ya Shilingi
Milioni 37 ili tuongeze mapato kwa kupima ardhi,” Alisema.
Hadi kufikia tarehe 12 mwezi Machi mwaka 2019
Manispaa ya Sumbawanga in wadaiwa wa makusanyo ya mapato ya ndani shilingi
milioni 45.97, Sumbawanga Vijiji Shilingi Milioni 756.17, Wilaya ya Kalambo
Shilingi Milioni 252.64 na Wilaya ya Nkasi Shilingi Milioni 290.95
0 comments:
Post a Comment