Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akitoa tamko
la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo
kwenye picha) wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo
katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi
wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe na wamwisho ni Mwenyekiti wa Chama
cha Magonjwa ya Figo nchini Dkt. Kisanga
Waandishi wa Habari waliojitokeza kumsikiliza Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika
Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
Na
WAMJW-DOM
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa kiasi cha Shilingi Bilion
3.4 ambacho kingetumika katika matibabu kwa Wagonjwa wa Figo nje ya Nchi.
Dkt.
Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea na Waandishi wa Habari
katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ikiwa ni Siku ya Figo Duniani
ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya
ya figo kwa kila mmoja kila.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho
kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya
nchi kwaajili ya matibabu.
“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama
tungewapeleka wagonjwa nje ya nchi
ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya
wagonjwa. 80 mpaka 100, wakati huduma
hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.”
Alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt, Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa sababu
zinazochangia magonjwa ya figo ni pamoja na uzito wa kupindukia (obesity),
matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara,kutokufanya
mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa dawa za kupunguza maumivu.
Aliendelea kusema kuwa, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu
ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha matatizo ya figo, magonjwa haya
yakitambuliwa mapema yanaweza kudhibitiwa kwa matibabu na kuepusha madhara
kwenye figo.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Kufikia Desemba
mwaka 2018, jumla ya vituo 28 vyenye jumla ya wagonjwa 1050 vilikuwa vikitoa
huduma ya usafishaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha,
Kilimanjaro na Dodoma.
Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema Serikali imepiga hatua kubwa
ya kuanzisha huduma za kupandikiza figo hapa nchini katika hospitali ya Taifa
Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Figo nchini
Dkt. Onesmo Kisanga amesema kuwa Ugonjwa wa Figo ni tatizo kubwa nchini huku
wananchi wengi wakiwa na uelewa mdogo juu ya athari na visababishi vya ugonjwa
huo.
Aidha Dkt. Onesmo amewataka wananchi kuacha tabia ya kunywa dawa
bila kupata ushauri wa kitaalamu hivyo kuepuka kuzalisha sumu mwilini na
kupelekea ugonjwa wa figo.
Hata hivyo Dkt. Onesmo Kisanga ameishukuru Serikali kwa
kuwaendeleza kimasomo wataalam kwenye upande wa matibabu ya figo ambao sasa
wamesambazwa sehemu mbali mbali ndani ya nchi kutoa huduma za matibabu.
Naye Dkt. Grace Maghembe Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya
Afya amesema ungojwa huu umekuwa ukiwaathiri zaidi wakazi wa mijini kuliko
vijijini kutoka na mfumo wa maisha uliopo sasa ambapo watu wengi wamekuwa
hawazingatii mtindo bora wa maisha kwa kutofanya mazoezi pamoja na kula chakula
bora.
Dkt. Maghembe amesema bado ipo changamoto kwenye matumizi ya dawa
za mitishamba ambazo bado hazijatambuliwa na kuthibitishwa huku akiwataka
wananchi kuwa waangalifu pia kwenye matumizi ya dawa hizo.
“Serikali
inatambua umuhimu wa tiba mbadala pamoja na matibabu ya
tiba za asili na ndio maana zipo taasisi za serikali zinazohusika kuzitambua
dawa hizo ni zipi na zina vitu gani na unatakiwa kutumia kwa kiwango gani” amesema Dkt
Maghembe nakuwataka watengenezaji wa dawa hizo kufuata taratibu zilizopo ili
kuthibitisha na kusajili dawa zao.
0 comments:
Post a Comment