Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ubalozi wa Marekani, imeandaa warsha kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kuripoti habari za uchaguzi inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Aprili 15, 2019 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Sengiyumva Gasirigwa amesema warsha hiyo iliyowakutanisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na binafsi imelenga kuimarisha mahusiano baina ya waandishi wa habari pamoja na mamlaka/ wasimamizi wa uchaguzi katika kuripoti habari za uchaguzi nchini kwa kuzingatia sheria.
Gasirigwa amesema pia warsha hiyo itawaongezea uelewa waandishi wa habari kutambua sheria mpya za vyombo vya habari pamoja na uchaguzi hatua itakayowasaidia kuripoti habari za uchaguzi kwa usahihi bila kuibua mkanganyiko katika jamii.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wamesema itawajengea uwezo wa kuimarisha mahusiano baina yao na wasimamizi wa uchaguzi ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na hivyo kuondokana na baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza nyakazi za uchaguzi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akitoa akitoa neno la ufunguzi kwenye warsha kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kuripoti habari za uchaguzi inayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Aprili 15, 2019 Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani, Japhet Sanga akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Idhaaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (V.O.A), Dkt. Mwamoyo Hamza akizungumza jambo kwenye warsha hiyo.
Dkt. Mwamoyo Hamza kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Redio Sauti ya Amerika akichangia jambo kwenye warsha hiyo.
Wakili James Marenga ambaye ni mmoja wa watoa mada akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, Joyce Shebe ambaye ni Mhariri kutoka Clouds Media Group akichangia jambo kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (kushoto), akimsikiliza mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, Joyce Shebe ambaye ni Mhariri kutoka Clouds Media Group (kulia).
Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Raziah Mwawanga akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John akizungumza jambo kwenye warsha hiyo.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, Flora Rugashoborola ambaye ni Mhariri kutoka Sahara Media Group akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mshiriki wa warsha hiyo, Moshy Kiyungi ambaye ni Meneja wa Kituo cha Radio cha Voice Of Tabara akichangia mada.
Mkurugenzi wa taasisi ya Internews, Wence Mushi akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo, Idda Mushi kutoka IPP Media akichangia jambo kwenye warsha hiyo.
Mmoja wa watoa mada, Paul Dotto Kuhenga ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano akichangia mada.
Baadhi ya watendaji kutoka taasisi ya MISA Tanzania, Andrew Marawiti (kushoto) ambaye niAfisa Utawala na Fedha pamoja na Neema Kasabuliro (kulia) ambaye ni Afisa Habari na Utafiti.
0 comments:
Post a Comment